January 21, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, October 13, 2016

Video Iliyochukuliwa 2005 imemponza Donard Trump.soma

Uchaguzi Marekani 2016: Trump 'alipapasa
wanawake kama pweza'
Wanawake wawili wameambia gazeti la New York
Times kwamba mgombea urais wa chama cha
Republican nchini Marekani Donald Trump
aliwashika kimapenzi bila idhini yao.
Mwanamke mmoja amesema mgombea huyo
alimshika matiti na kujaribu kuingia mkono wake
chini ya sketi yake wakiwa kwenye ndege miongo
mitatu iliyopita.
Wa pili anasema Bw Trump alimpiga busu bila
yeye kutaka katika jumba la Trump Towers
mwaka 2005.
Maafisa wa kampeni wa Trump wamesema
"makala hii yote ni hadithi ya kubuni".
Gazeti la New York Times limeanzisha kampeni
"ya uongo, na iliyoratibiwa kumharibia jina
kabisa", taarifa ya maafisa wa Trump imesema.
Jessica Leeds, 74, kutoka Manhattan, ameambia
gazeti hilo kwamba alikuwa ameketi karibu na Bw
Trump sehemu ya abiria wa hadhi ya juu kwenye
ndege wakielekea New York pale alipoinua
sehemu ya kupumzishia mkono kitini na akaanza
kumshika.
Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 38
wakati huo.
"Alikuwa kama pweza .... mikono yake ilinishika
kila pahali," anasema. "Ulikuwa ni unyanyasaji."
Rachel Crooks alikuwa mpokezi wa wageni katika
kampuni ya kuuza ardhi ya nyumba katika jumba
la Trump Tower, wakati huo akiwa na miaka 22.
Anasema alipigwa busu la lazima na Bw Trump
nje ya lifti ya jengo hilo.
"Ilikuwa vibaya sana," Bi Crooks ameambia New
York Times.
"Niliudhika sana kwamba alidhani nilikuwa sina
maana kiasi kwamba angefanya hivyo (bila hiari
yangu)."
Wawili hao hata hivyo hawakuripoti visa hivyo
kwa maafisa wa serikali.
Hata hivyo, wanasema waliwaambia marafiki na
jamaa zao yaliyojiri.
Bi Leeds anasema alikasirika sana na alitatizika
kimawazo baada ya Bw Trump kumgusa.
Anasema mara moja aliondoka eneo la abiria wa
hadhi na kwenda kuketi eneo la abiria wa
kawaida.
Maafisa wa kampeni wa Clinton wamesema
simulizi hizo za kuogofya kwenye New York
Times zinatilia mkazo "kila kitu ambacho tunajua
kuhusu jinsi Donald Trump huwachukulia
wanawake".
'Kumshika makalio'
Hayo yakijiri, Mindy McGillivray naye ameambia
gazeti la Palm Beach Post kwamba akiwa na
miaka 23 , Bw Trump alimshika makalio katika
kilabu chake cha Mar-a-Lago club jimbo la
Florida mwaka 2003.
Anasema alikuwa amesimama karibu na
mchumba wake wa wakati huo Melania Knauss.
Bi McGillivray, ambaye kwa sasa ana miaka 36,
anasema hakuripoti kisa hicho kwa polisi.
Lakini mwenzake, mpiga picha Ken Davidoff,
aliambia gazeti hilo kwamba mwanamke huyo
alimwita kando siku hiyo na kumwambia: "Donald
amenishika makalio sasa hivi".
Maafisa wa Trump wanasema madai ya Bi
McGillivray hayana ukweli wowote.
Wanawake wote watatu wamesema wanaunga
mkono Bi Clinton.
Ijumaa wiki jana, video iliyopigwa mwaka 2005
ilitokea na kumuonyesha Bw Trump akinena
maneno ya kuwadhalilisha wanawake na kuongea
kuhusu kuwapapasa wanawake.
Aliomba radhi kuhusu matamshi hayo, lakini
akasema yalikuwa mazungumzo ya mzaha
faraghani.
Viongozi wengi wakuu wa Republican, akiwemo
Spika Paul Ryan, wameshutumu matamshi hayo.
Bw Ryan alisema hatamtetea tena Bw Trump.
# BBC

0 comments :

Post a Comment

Back To Top