Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, November 17, 2016

Afisa wa forodha wilayani Tarime afikishwa Mahakamani.soma zaid

AFISA WA FORODHA WILAYANI TARIME
AFIKISHWA MAHAKANI.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa
Takukuru mkoani Mara,imemfikisha
mahakamani Afisa forodha wa mamlaka ya
mapato Tanzania TRA,kituo cha Sirari EZEKIEL
GISUNTE kwa kosa la kudai na kupokea rushwa
ya shilingi milioni kumi na tano toka kwa
mfanya biashara wa vifaa vya ujenzi aliyekuwa
akipitisha bidhaa zake mpakani hapo.
Kamanda wa kikosi cha kuzuia na kupambana na
Rushwa mkoani Mara,Holle Makungu
ameyasema hayo muda mfupi baada ya afisa
huyo kupandishwa na kusomewa mashitaka
mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya
wilaya ya Tarime Mh. Martha Mpanze na
kisisitiza kuwa iwapo Gisunte angefanikiwa
angeitia hasara serilikali ya shilingi milioni 48.
Mpaka wa Sirari uliopo wilayani Tarime mkoani
Mara,umekuwa ukikusanya mapato zaidi ya
shilingi bilioni 75.5 kwa mwaka kutokana na
malipo ya kodi za bidhaa ziingiazo nchini
kupitia mpaka huo.
Kutokana na hali hiyo,taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa mkoani humo,imeweza
kubaini na kumfikisha mahakamani afisa
forodha wa mamlaka ya mapato katika mpaka
huo, Ezekiel Gisunte,kwa tuhuma ya kudai na
kupokea rushwa ili kumpunguzia kodi
mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi.
Aidha kamanda Holle anasema kuwa Afisa huyo
akijua yeye ni mtumishi wa serikali kupitia
mamlaka hiyo,alidanganya kwa kutengeneza
account nyingine ili asibainike.
Awali mkuu wa wilaya ya Tarime,Grolius Luoga
na mkuu wa mamlaka ya mapato mkoani
Mara,wakizungumzia tatizo hilo walimtaja
Gisunte kwenda kinyume na maadili ya utumishi
wa umma.
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoani Mara
kupitia mpaka wa Sirari imedaiwa kupoteza
mapato mengi kutokana na watumishi wasio
waadilifu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top