Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, November 16, 2016

Wazir Mbarawa azinduka bodi mpya TRLsoma zaid


Waziri wa Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi, Prof.
Makame Mbarawa leo amezindua bodi mpya ya
Shirika la Reli Tanzania (TRL) na kuitaka kufanya
kazi kwa ushirikiano mkubwa na wafanyakazi
wote wa shirika hilo.
Amsema hayo alipokuwa katika uzinduzi huo
makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es salaam,
na kuisisitiza bodi hiyo kuwa waadilifu na
wazalendo, ameongeza kuwa kama mtu
akishindwa kusimamia uadilifu basi hana nafasi
ya kufanya kazi katika shirika hilo.
Aidha, Mbarawa amesema TRL inajukumu kubwa
la kukabiliana na soko la ushindani ambalo
linashikiliwa na malori makubwa ya usafirishaji,
amesema kuwa kazi kubwa ni kutoa huduma
nzuri ambazo zitawashawishi wateja kutumia
usafiri huo ambapo itasaidia kujipatia masoko
mengi zaidi.
Walioteuli katika bodi hiyo ya TRL ni pamoja na
aliyekuwa mkuu wa chuo mstaafu cha DIT, Prof.
John Wajanga Kandoro ambaye ndiye mwenyekiti
wa bodi hiyo, wengine ni Linford Mboma alikuwa
mwenyekiti TRC, Miriam Mwanilwa kutoka Ofisi
ya Rais bodi ya mishahara, Martha Maeda kutoka
TIB, Mhandisi Charles Mvungi kutoka TIB,na
Mashaka Mabuyu ambaye ametoka WFB.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top