Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, November 17, 2016

Mahakama kanda kuu ya Arusha imeomba siku 5 juu ya kutoa dhamana ya Mbunge Lema.soma zaid

Harakati za kumpatia dhamana mbunge wa
Arusha Mh Godbless Lema anayekabiliwa na kesi
ya uchochezi zimeendelea kugonga ukuta baada
mahakama kuu kanda ya Arusha kusikiliza hoja
za pande zote na kuahidi kuzitolea uamuzi baada
ya siku tano.
Hatua hiyo imekuja baada ya mawakili wa pande
zote kuwasilisha hoja zao kila upande ukitetea
hoja yake mbele ya jaji wa mahakama hiyo Mh
Sekela Moshi.
Jopo la mawakili wanaomtetea Mh Lema
wakiongozwa na wakili msomi Peter Kibatala,
John Malya, Adamu Jabiri, Sheki Mfinanga na
Charles Adirian Faraji Mangula walimweleza Mh
jaji Sekela Moshi kuwa taratibu za kuweka
pingamizi zilikiukwa hivyo shauri hilo litupiliwe
mbali na mteja wao apewe dhamana.
Kwa upande wa mawakili wa serikali
walioongozwa na wakili msomi Paul Kadushi na
Mosese Marandu nao waliendelea kushikilia na
kutetea hoja yao kuwa mtuhumiwa hastahili
kupewa dhamana kwa sababu ambazo
walishaziwasilisha na kwamba pingamizi
waliloweka linakubalika kisheria na kama
mtumiwa anaona kuwa lina mapungufu
anapashwa kukata rufaa na sio kuwasilisha barua
kama alivyofanya.
Baada ya mvutano wa mjadala mkali wa kisheria
wa mawakili hao wa pande mbili Mh jaji Sekela
Moshi akaiambia mahakama kuwa kulingana na
uzito wa hoja anahitaji muda wa kuzipitia na
kwamba atatoa maamuzi siku ya jumanne tarehe
22 .11.2016.
Kufuatia maamuzi hayo mtuhumiwa Lema
alirudishwa tena mahabusu kusubiri siku ya
tarehe 21.11.2016 atakapopandishwa kizimbani
tena kuendelea na kesi yake ya msingi ya
uchochezi na maneno ya kashifa kwa viongozi
wa serikali na pia siku ya tarehe 22 /11/2016
atakapofikishwa mahakamani hapo kujua hatma
yake ya dhamana.
Wakati wote kesi ilipokuwa inaendelea ulinzi
uliimarishwa ndani na nje ya mahakama na wote
waliochele walikatazwa kuingia wakati kesi
inaendelea wakiwemo viongozi waandammizi wa
Chadema kutoka makao makuu walioongozwa na
mjumbe wa halmashauri kuu vijana taifa Joseph
Kasambala.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top