Baraza la waislamu nchini Marekani wamesema hawataondoka marekani licha ya Trump kushinda Urais.soma zaid
Baraza la Waislamu nchini Marekani
limemhimiza Donald Trump kuzingatia haki na
usawa wa wananchi wote bila ya ubaguzi wa
kidini kufuatia ushindi wake kwenye uchaguzi
wa rais.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mji
mkuu wa Washington, mkuu wa baraza hilo
Nihad Awad alitoa wito kwa rais huyo mpya
kuzingatia haki za wananchi wa Marekani
wakiwemo Waislamu.
Akikumbushia matamshi ya chuki na ubaguzi
dhidi ya Waislamu aliyotoa Donald Trump wakati
wa kampeni, Awad alisema, ''Waislamu wa
Marekani wataendelea kuishi nchini. Hatutoenda
popote na wala hatutokaa kimya kuhusu suala
hili.''
Awad aliongezea kusema kuwa baraza hilo
litaendelea kupigania haki za Waislamu na
uhuru wao kama ilivyokuwa hapo awali ili
kumaliza unyanyasaji.
Awad pia alitoa wito kwa Waislamu wote
wanaoishi nchini humo kuondoa hofu huku
akiwakumbusha haki zao ambazo ni sawa na
wananchi wengi wa Marekani.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, Donald Trump
alikuwa akikshifiwa kwa matamshi yake ya
ubaguzi na kutaka kuzuia Waislamu kuingia
Marekani huku akitoa wito wa kufungwa kwa
misikiti.
0 comments :
Post a Comment