Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, November 10, 2016

Rais Shein amewaapisha manaibu waziri wapy ikulu ya zanzibar.soma zaid

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo
amewaapisha Manaibu Waziri wapya ambao
aliwateuwa hivi karibuni kushika nyadhifa katika
Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Walioapishwa ni Mihayo Juma Nhunga kuwa
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili
wa Rais, Shamata Shaame Khamis, Naibu Waziri
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za
Mitaa na Idara Maalum za SMZ na Shadya
Mohamed Suleiman, kuwa Naibu Waziri wa Kazi,
Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na
Watoto.
Hafla ya kuwaapisha viongozi hao ilifanyika
Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi
mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi hao ni Makamo wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mohammed Aboud, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na
Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheri.
Wengine ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee,
Vijana, Wanawake na Watoto Maudline Castico,
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan
Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Kadhi
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa
Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed
Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa
Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa
Rais wa Zanzibar, Wakuu wa Vikosi vya SMZ na
viongozi wengine wa Serikali.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top