Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, November 16, 2016

Campuni ya Selcom ya China yasababisha taharuki ya ukosefu wa maji Dodoma.soma zaid

Wakazi wa mtaa wa Area A manispaa ya
Dodoma wamekosa huduma ya maji kwa
zaidi ya wiki tatu baada ya kampuni ya
Selcom kutoka uchina inayojenga mitaro
ya barabarani katika eneo hilo kukata kwa
makusudi mabomba ya maji na
kujiunganishia kinyemela kwa ajili ya
matumizi ya ujenzi bila kufuata utaratibu.
Wakizungumza baada ya maofisa wa
mamlaka ya maji na usafi wa mazingira
mjini Dodoma DUWASA kwa kushirikiana
na jeshi la polisi kuvamia eneo la ujenzi
la wakandarasi hao baada ya kupata
taarifa kutoka kwa wasamaria wema
wakazi hao wanadai tangu kuanza kwa
ujenzi huo wamekosa huduma ya maji hali
iliyowasababishia usumbufu mkubwa na
kuongeza gharama za maisha.
Ester Galinoma ni kaimu afisa mapato wa
DUWASA ambaye anasema kitendo
kilichofanywa na wakandarasi hao
kimeisababishia mamlaka hiyo hasara
kubwa na hatua kali zitachukuliwa dhidi
yao huku mkuu wa kitengo cha
mawasiliano kwa umma akiwataka
wananchi kuwa mabalozi wazuri kwa
kuwafichua wezi wa maji ili huduma hiyo
iboreshwe mjini Dodoma.
Kwa upande wake msimamizi wa ujenzi
katika eneo hilo raia wa uchina hakuweza
kutoa ufafanuzi wowote kuhusu tukio hilo
kutokana na kutofahamu lugha ya
kiswahili wala kingereza.
Chanzo: ITV

0 comments :

Post a Comment

Back To Top