Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, November 30, 2016

CHADEMA yaapa haitokubali kudhulumiwa tena kataka uchaguzi wa mwaka2020.soma zaid

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji
amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa
namna yoyote katika uchaguzi wa mwaka
2020.
Dk. Mashinji amesema hayo huku akimtolea
mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na
kuongeza kuwa kuna mambo hutokea bila
kutarajia lakini watapambana kwa kila hali,
“Huu ni uchaguzi kuna mtu alitarajia haya
yaliyofanywa na Jecha? hii inaonyesha kwenye
nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki, wewe
umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya
tena mara ya pili kibabe,tukalalamika, badala ya
kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme
kokote kule” alisema Mashinji.
Aidha, akiongelea utawala wa Rais Magufuli
,Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji
mkubwa wa utawala bora na matokeo yake
yeye ndio amekuwa kila kitu, ameongeza kuwa
wakati anaanza mapambano na rushwa aliamini
kwamba angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini
imekuwa tofauti.
Hata hivyo, Mashinji ameongeza kuwa katika
mwaka mmoja wa Rais Magufuli, amesema
ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya
kupiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja
na shughuli zote za kisiasa nchini kwa kile
alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.chanzo mpekuzi blog

0 comments :

Post a Comment

Back To Top