Chama cha CHADEMA kimempongeza rais mteule wa Marekani Donard Trump.soma zaid
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
(CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA –UCHAGUZI MKUU WA
MAREKANI.
· Pongezi kwa Rais Mteule
· Ni ushindi wetu IDU
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kinawapongeza wananchi wa
Marekani kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya
amani hapo tarehe 08.11.2016, na kukamilisha
kampeni za kumpata kiongozi wa Nchi hiyo.
Tunapenda kumpongeza Rais Mteule Mhe.Donald
Trump na Chama chake cha Republican ambao
ni wanachama wa IDU kwa ushindi wa kihistoria
walioupata , na zaidi tunampongeza rais mteule
Trump kwa hotuba yake ya awali ya
kuwashukuru wananchi wa Marekani na hasa
aliposema kuwa anaahidi kwa wananchi wote wa
Marekani kuwa anaenda kuwa rais wa wote, na
kuwa hilo ni jambo la umuhimu wa kipekee
kwake .
“I pledge to every citizen of our land that I will
be President for all Americans and this is so
Important to me”
Ushindi huu ni ushindi wetu sisi wanachama wa
Jumuiya ya Kimataifa ya Kidemokrasia
(International Democratic Union-IDU) na unatuma
salaam nzito kwa Madikteta popote pale walipo
kuwa utawala mpya wa Marekani hautavumilia
kuona Madikteta ambao wanaminya Demokrasia
na Haki za Binadamu, kama alivyoahidi wakati
wa Kampeni zake .
Tunaahidi kumpa ushirikiano wote kwenye vikao
vya IDU ambavyo sisi tunashiriki kama
wanachama wa umoja huu na tutampatia kila
aina ya taarifa sahihi kadiri ya uwezo wetu
kuhusu hali ya Haki za Binadamu na Demokrasia
nchini Tanzania na Barani Afrika.
Mwisho, tunampongeza Hillary Clinton kwa
kufanya kampeni za kihistoria na kukubali
matokeo ya kura .
Imetolewa leo tarehe 09.11.2016
John Mrema –Mkurugenzi wa Itikadi,
Mawasiliano na Mambo ya Nje
0 comments :
Post a Comment