Posho kwa watumishi wa umma hazijafutwa.soma zaid
SERIKALI imesema si kweli kuwa posho kwa
watumishi wa taasisi za umma zimefutwa, bali
marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma
yamelenga kuipunguzia serikali gharama na
tayari hatua zimechukuliwa ambapo kuanzia
Julai mwaka huu, hakuna mkuu wa taasisi
anayelipwa zaidi ya Sh milioni 15.
Aidha, imesema hakuna Sheria ya Utumishi wa
Umma wala yoyote iliyovunjwa na Rais John
Magufuli, alipofanya uteuzi wa wakurugenzi
watendaji kwa kuwa Katiba ya nchi, inamruhusu
kufanya hivyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati
wakifafanua hoja za serikali wakati wa
majadiliano ya Muswada wa Sheria ya
Mabadiliko ya Sheria mbalimbali Namba 3 wa
mwaka 2016, mawaziri wa wizara mbalimbali
walisema Rais anaongoza nchi kwa misingi ya
sheria.
Mawaziri hao walikuwa wakijibu hoja za
wabunge, ikiwemo hoja ya Msemaji wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Katiba na Sheria,
Tundu Lissu kuhusu muswada huo baada ya
kueleza kuwa Rais amevunja sheria za utumishi
wa umma, za uchaguzi kuteua baadhi ya
makada wa CCM kuwa wakurugenzi watendaji,
akijua kuwa watahusika kusimamia uchaguzi na
hawatatenda haki kwa vyama vingine.
Akieleza kuhusu hoja hiyo, Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye,
alisema “Katika katika Ibara ya 36, inampa Rais
mamlaka ya kufuta, kuanzisha na kuteua.
Hakuvunja Katiba hata kidogo, amechagua watu
watakaomsaidia kufikia malengo na ahadi
alizotoa.”
Nape alitaka kauli hizo zipuuzwe, kwani zina
lengo la kupoteza ajenda na kuwataka
Watanzania kumuamini Rais katika kuwafikisha
katika Tanzania mpya kiuchumi.
Akijibu hoja hiyo, Nape alisema, “Ajenda ya
Serikali ya Awamu ya Tano ni kurejesha
nidhamu ya utumishi wa umma. Watanzania
walituamini katika hilo na tunalitekeleza,
wapinzani wanataka kuzuia tusitekeleze ajenda
yetu”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella
Kairuki alisema nia ya serikali ni kuwianisha
mishahara na posho ni njema kupunguza
gharama na kuanzia Julai hakuna mkuu wa
taasisi anayelipwa zaidi ya Sh milioni 15.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George
Masaju katika majumuisho alisema kulikuwa na
malalamiko makubwa kuhusu tofauti ya
mishahara kati ya mtu wa chini na wa juu, hivyo
shera hiyo imelenga kuweka usawa bila
upendeleo.
0 comments :
Post a Comment