CIA yamuimonya TRUMP kuhusu mpango wake.soma zaid
Shirika la Kijasusi Nchini Marekani CIA limeingiwa
na wasiwasi Juu ya Mipango ya Rais Mteule wa
Marekani Donald Trump, ya kusitisha
makubaliano ya mpango wa nyuklia na Iran na
kusema kuwa kufanya hivyo itahatarisha Usalama
wa Taifa hilo kubwa lenye nguvu duniani.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo,
John Brennan alipokuwa akifanya mahojiano na
vyombo vya habari nchini humo, ambapo
amemshauri Rais huyo mpya kuwa na tahadhari
kubwa kuhusu ahadi na matamko yake ambayo
amekuwa akiyatoa kulingana na mustakabari wa
sera zake.
Aidha, Brennan amesema ahadi za Trump kuhusu
kuwa na mahusiano ya karibu na Urus, ni hatari
zaidi kwani nchi hiyo inahusika na upotevu wa
amani nchini Syria .
Brennan alitaja mambo machache ambapo
alisema kuwa utawala mpya unatakiwa
kuyazingatia kwa busara na hekima, ikiwemo
lugha inayotumiwa kuhusu Ugaidi, Uhusiano na
Urusi, mpango wa kinyuklia wa Iran na siri za
Shirika hilo hutekelezwa
0 comments :
Post a Comment