Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, November 30, 2016

Omar el Bashir huko tayar kushirikiana na rais mteule wa marekan Donard Trump.soma zaid

Kiongozi wa Sudan Omar el Bashir
amempongeza rais mteule wa Marekani Donald
Trump akisema kuwa itakuwa rahisi kushirikiana
naye, kulingana na gazeti la Emirati al Khaljee.
''Bw Trump anaangazia maslahi ya raia wa
Marekani, ikilinganishwa na wale
wanaozungumzia kuhusu demokrasia ,haki za
kibinaadamu na uwazi'',alisema rais Bashir katika
mahojiano na gazeti hilo.
Aliongezea kwamba: Tunaweza kushirikina na
watu wenye sura mbili lakini huyu hapa mtu
mwenye uwazi wa anajua anacholenga.
''Nina hakika itakuwa rais kushirikiana na Trump
ikilinganishwa na wengine kwa sababu ni mtu
anayeangazia maswala moja kwa moja na
mfanyibiashara ambaye anaangazia maslahi ya
anaoshirikiana nao'',alisema Bashir.
Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya ICC
kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari
katika eneo la Drafur amekana mashtaka hayo.
Alichukua mamlaka mwaka 1989 kupitia
mapinduzi na ameshutumiwa kwa kuwa na
uongozi wa kiimla tangu wakati huo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top