Breaking News
Loading...

Advert

Monday, December 5, 2016

Rais magufuli ataja tarehe ya ndege 4 mpya kukamilika.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko ya
Afrika wa Kampuni ya utengenezaji wa ndege ya
Boeing yenye makao yake nchini Marekani Bw.
Jim Deboo.
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli
Mazungumzo hayo ambayo ni sehemu ya juhudi
za Serikali za kununua ndege kubwa kutoka
kampuni hiyo, yamefanyika Ikulu Jijini Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu
Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto
James.
Baada ya Mazungumzo hayo Rais Magufuli
amesema Serikali yake ya Awamu ya Tano
imedhamiria kununua ndege nyingine nne
zikiwemo ndege kubwa 3 ambazo zitasaidia
kuinua uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii
kuja hapa nchini moja kwa moja kutoka nchi zao.
"Sisi hapa tunazungumza kuwa watalii hawajafika
hata milioni 2 kwa mwaka, lakini nchi kama
Morocco inapata watalii zaidi ya milioni 12 kwa
mwaka, hii yote ni kwa sababu hatuna mashirika
ya ndege ya kwetu, watalii wakitaka kuja hapa ni
lazima waje kwa kuungaunga, wafikie nchi
nyingine halafu ndipo wapate moyo wa kuja huku,
licha ya kwamba sisi Tanzania ni miongoni mwa
nchi 5 duniani zenye maeneo mazuri yenye utalii.
"Kwa hiyo niwaombe tu Watanzania wapende
mali zao, kwa sababu wakati mwingine
nikiangalia mitandao na magazeti ni ajabu huwezi
kuamini kama hao ni Watanzania, unakuta
wanasifia tu ndege za watu wengine na
wanazibeza za kwao" amesisitiza Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ametaja aina ya ndege mpya
ambazo Serikali itazinunua kuwa ni ndege 1 aina
Bombardier Q400 Dash 8 NextGen inayotarajiwa
kufika nchini Mwezi Juni 2017, ndege 2 aina ya
Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua
kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa
kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018 na
ndege moja aina ya Boeing 787 Dash 8 Dream
Liner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 na
inayotarajiwa kuwasili nchini Juni, 2018. Malipo
ya awali kwa ndege hizi yameshafanyika.
Dkt. Magufuli amewataka Watanzania kuunga
mkono juhudi hizi za Serikali zenye lengo la
kuinua utalii na kuimarisha uchumi wa nchi.
"Tumeleta ndege aina ya Bombardier hapa,
zimepunguza gharama za safari mfano kutoka
Dar es Salaam hadi Mwanza, sasa wanalipa kati
ya 160,000/ hadi 200,000/- wakati nauli ilishafika
Shilingi laki 8 na kitu, lakini watu wengine
utakuta wanazungumzazungumza wee maneno
ya hovyo kwa kutumiwa, tumeshaamua na
tutafanya hivyo" amesisitiza Rais Magufuli.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top