Upatikanaji wa maji Dar umefikia asilimia 72.soms zaid
SERIKALI imesema kuwa maji upatikanaji wa
maji katika mkoa wa Dar es Salaam umefikia
asilimia 72 na kwamba Mpango wa Maendeleo
ya sekta hiyo wa miaka mitano ijayo
utawezesha kufikia asilimia 95.
Kwa upande wa vijijini, maji yanapatikana kwa
asilimia 72 sawa na Dar es Salaam, huku mijini
yakipatikana kwa asilimia 86 na katika wilaya
yanapatikana kwa asilimia 60.
Hayo yalibainishwa juzi na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mbogo
Futakamba, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha
Tunatekeleza kinachorushwa na TBC 1.
Futakamba alisema katika awamu ya kwanza ya
mpango huo, walifanikiwa kutekeleza miradi
1,310 na kwamba Julai mwaka huu wameanza
mradi huo wa pili wa kuhakikisha upatikanaji wa
maji vijijini, mijini, usafi wa mazingira na utunzaji
wa rasilimali za maji.
“Tunahakikisha kwamba kila Mtanzania anapata
majisafi na salama na hii sekta ichangie katika
ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya viwanda. Hizi
takwimu ni sahihi kwani tumetumia zile za
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
zilizoonesha ni kwa namna gani watu walifikiwa
na huduma hiyo,” alisema.
Alifafanua kuwa vitu vinavyokwamisha
utekelezaji wa miradi hiyo ni changamoto
mbalimbali, ikiwemo uwekezaji katika
miundombinu hiyo, uharibifu na mfumo wa chini
wa upatikanaji wa maji kuwa ya chumvi hivyo
hakuna wananchi ambao wako tayari kutumia.
Alisema kwa Dar es Salaam, maji yanapatikana
lita zaidi ya milioni moja kutoka Ruvu Juu huku
Ruvu Chini ikitoa maji zaidi ya lita milioni 270.
Akizungumzia mradi wa Kidunda uliopo
Morogoro ambao pia utasambaza maji kwenye
mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam,
alisema utekelezaji wake umefanyika na
unasaidia kudhibiti mafuriko, kupeleka maji
katika mto Ruvu.
Alisema masuala ya kitaalamu yamekamilika.
Aliongeza kuwa pamoja na kuweka sheria kwa
watu wanaoharibu miundombinu hiyo,
wameanzisha jumuiya za watumiaji maji ambao
wanapewa mafunzo ya kuangalia masuala ya
utawala, utunzaji fedha na utunzaji miundombinu
na kudhibiti uharibifu ambao mara nyingi
hufanywa na wananchi.
Kwa mujibu wa Futakamba, hali hiyo imesaidia
sana kwa kuwa wananchi wanajua kwamba huo
ni mradi wao na ukitokea uharibifu wanakuwa
tayari kufanya matengenezo katika maeneo
yaliyoharibiwa.
0
0 comments :
Post a Comment