Shule za binafisi zitakazo kiuka agizo la serikali zitafutiwa usajiki.soma zaid
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi imesema itazifutia usajili
shule zote binafsi, ambazo zitabainika kukiuka
agizo la serikali la kuzitaka shule zote nchini
kuwa na mihula miwili ya masomo badala ya
mitatu, ambayo imekuwa inafuatwa na shule
zisizo za serikali.
Ili kutekeleza azma hiyo, wizara hiyo imewaagiza
wakaguzi wa shule pamoja na maofisa elimu wa
wilaya, kufanya ukaguzi katika shule binafsi
zilizoko katika meneo yao; kubaini kama kuna
shule binafsi zilizokaidi kutekeleza Waraka wa
Elimu Namba Moja wa Mwaka 2015.
Kaimu Kamishna wa Elimu, Venance Manori
alisema wizara yake ilitoa waraka huo ikiwa ni
njia ya kukazia Waraka wa Serikali Namba 5 wa
Mwaka 2012 ambao ulikuwa unaelekeza mihula
ya masomo kwa shule za sekondari na vyuo vya
ualimu, ifanane ili kuepusha usumbufu kwa
walimu na kwa wanafunzi.
Waraka huo ulifafanua kuwa kila muhula utakuwa
na likizo fupi na likizo ya mwisho wa muhula na
siku za masomo kwa mwaka zitakuwa ni 194.
Pia waraka huo unataka siku za michezo ya
Umitashumita na Umiseta kwa shule za msingi
na sekondari, zifanane kwa shule zote. Lakini
pamoja na kuwepo waraka huo, baadhi ya shule
zisizo za serikali zimeendelea kufuata mihula
mitatu.
Baadhi ya shule katika ripoti za wanafunzi za
mwezi Desemba kwenda kwa wazazi,
wameonesha kuwa mwaka ujao wa masomo
utakuwa wa mihula mitatu na nyingine minne.
“Wizara ilifanya utafiti na kujiridhisha kuwa
haiwezekani shule zinazotoa elimu msingi kuwa
na mihula mitatu, ndio maana tukataka nchi
nzima tuwe na mfumo ambao unafanana ili
kuepusha usumbufu kwa walimu na wanafunzi,”
alisema Manori.
Alisema kwanza haamini kama kuna shule
ambazo sio za serikali ambazo bado zinafuata
mihula mitatu, na akaongeza kuwa kama zipo na
wizara hiyo ikapata uthibitisho, lazima hatua za
sheria zichukuliwe na hatua mojawapo ni
kuzifuatia sheria.
“Ule waraka ulisambazwa kwa mamlaka zote za
utekelezaji ukiwemo umoja wa shule binafsi na
taasisi inayosimamia shule za dini ya Kikristo na
shule za Baraza la Kiislamu, hivyo hakuna
kisingizio cha mtu kutopata huo waraka, hivyo
lazima wautekeleze,” alieleza Manori.
Hata hivyo, pamoja na waraka huo baadhi ya
shule binafsi, zimekaidi agizo hilo na zimeendelea
kufuata mihula mitatu, jambo ambalo ni kwenda
kinyume cha maagizo hayo ya serikali. Kutokana
na ukaidi huo, Manori alisema kuanzia mwakani,
shule ambazo zitabaini kukaidi agizo hilo
zitafutiliwa usajili.
Manori alisema wakaguzi wa elimu hiyo ndio kazi
yao kuhakikisha kwamba maagizo yote ya serikali
yanafuatwa. Pia alitoa mwito kwa wazazi ambao
wanapata maelekezo ya mihula ya shule
inayoenda kinyume cha maagizo ya serikali,
waripoti suala hilo kwa malofisa elimu wilaya na
wakaguzi wa shule.
“Sio kwamba wazazi wote waje hapa wizarani
kulalamika, wale wanaoweza walete malalamiko
hayo na walioko mikoani waende kwa maofisa
elimu wa mikoa, wilaya na wakaguzi wa shule ili
hatua stahiki ziweze kuchukuliwa,” alifafanua
Kamishna huyo.
Alisema hivi karibuni wizara yake itatoa kalenda
ya masomo na mihula, itakayofuatwa na shule
zote zinazotoa elimu msingi, kama walivyotoa
kalenda ya masomo katika mwaka huu.
Pia alikiagiza Chama cha Wamiliki wa Shule na
Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Baraza la
Waislamu Tanzania (Bakwata), Tume ya Huduma
za Kijamii ya Kikristo ambao ndio wanasimamia
shule ambazo sio za serikali nchini, kuhakikisha
wanachama wao wanatekeleza waraka huo wa
serikali.
Msimamo wa Tamongsco Katibu Mkuu wa
Tamongsco, Benjamin Nkonya alipoulizwa kutoa
maoni yake alisema, “Niko kwenye mkutano,
lakini sisi bado hatukubaliani na waraka huo wa
serikali, nitumie e-mail yako nitakuandikia sababu
za kupinga waraka huo.”
Hata hivyo, Nkonya baadaye alituma nakala ya
barua iliyoandikwa na yeye kwenda kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi kumwomba shule binafsi
ziendelee kutumia mihula mitatu kwa sababu
inarahisisha ukusanyaji wa ada kutoka kwa
wazazi na walezi.
Nkonya pia alisema Tamongsco imetaka mihula
mitatu kwa sababu mfumo huo unaruhusu baadhi
ya shule kufungwa Aprili wakati huo ambao huwa
na mvua za masika katika baadhi ya sehemu
nchini, mvua inaharibu barabara na hivyo
kusababisha gharama kuongezeka kutokana na
magari ya shule kuharibika.
Alisema Tamongsco pia imebaini kuwa mihula
hiyo mitatu, inatoa fursa kwa wenye shule
kuzifanyia matengenezo shule zao.
0 comments :
Post a Comment