Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, December 6, 2016

Vigogo 5 wa Taasafu wasimamishwa kazi.soma zaid


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah
Kairuki amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf),
kuwasimamisha kazi maofisa waandamizi watano
wa mfuko.
Maofisa hao ni wanaosimamia mpango huo
pamoja na Meneja wa Uratibu na Mkurugenzi wa
Uratibu kutokana na kushindwa kusimamia
mpango wa kunusuru kaya masikini.
Kairuki alisema maofisa hao ndio viongozi
wasimamizi wakuu wa mpango huo katika
Awamu ya Tatu ya Tasaf na wamesimamishwa
kupisha uchunguzi wa jinsi walivyohusika
kuvuruga utekelezaji wa mpango huo hadi kufikia
kuandikisha kaya zisizo na sifa ufanyike.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar
es Salaam, Kairuki alisema ameshauriana na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na tayari
ameshaelekeza waratibu wa Tasaf wa wilaya pia
wasimamishwe kazi.
“Nimemwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf
awasimamishe kazi mara moja na kuendelea na
hatua nyingine za kinidhamu dhidi ya maofisa
washauri 106 walioko kwenye halmashauri
walioshindwa kufuatilia na kusimamia mpango
huu mpaka kusababisha kaya zisizostahili
kuingizwa kwenye mpango na kuendelea kulipwa
isivyostahili,” alisema Kairuki.
Aidha alisema ameagiza ufanyike uchunguzi wa
kina kubaini ushiriki wa maofisa hao na kuchukua
hatua stahiki kwa wale watakaothibitika
kuhusika.
Aidha ametaka uchunguzi huo ukamilike ndani ya
mwezi. Karuki alisema baada ya uhakiki
kufanyika kaya 55,692 zimeondolewa kwenye
mpango kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
vifo, kaya kuhama kijiji, kutojitokeza mara tatu
mfululizo kupokea ruzuku, kuwa wajumbe wa
kamati mbalimbali, wastaafu, viongozi na
watumishi wa umma.
Alisema kuanzia Januari 2014 hadi Septemba
2016, Sh 6,427,110,309 zimeokolewa kwa kaya
42,035 zilizoondolewa kwa kipindi hicho na kwa
kuwa kazi hiyo ni endelevu kuanzia Oktoba 2016
wakikamilisha kuziondoa kaya zisizostahili kiasi
hicho cha fedha kinaweza kubadilika.
Hata hivyo amewaagiza Tasaf kuhakikisha
wanaendelea kushirikiana na halmashauri
kuongeza udhibiti wa fedha wakati wa malipo na
kuhakikisha fedha zinalipwa kwa kaya zenye sifa
peke yake.
Aidha, amewaagiza Tasaf kuendelea kushirikiana
na halmashauri zote kukamilisha kazi ya uhakiki
wa nyumba kwa nyumba katika halmashauri zote
nchini kabla ya malipo yanayofuata ya Januari/
Februari 2017 kufanyika.chanzo habar leo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top