Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, December 7, 2016

Msajili wa Hazina Ndg.Lawrence Mafuru atumbuliw.soma zaid

Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa
Msajili wa Hazina Ndg.Lawrence Mafuru na
kumteua Dr.Osward Mashindano kuwa Msajili
mpya Hazina. Katika taarifa iliyotolewa na
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu inasema Mafuru
atapangiwa kazi nyingine.
Siku chache zilizopita Mafuru alinukuliwa na
vyombo vya habari akisema kuwa hakuna
mtumishi yeyote wa umma aliyewahi kulipwa
mshahara wa TZS Mil.40 kwa mwezi. Kauli ya
Mafuru ilitafsiriwa kuwa inapingana kauli ya Rais
JPM aliyoitoa miezi kadhaa iliyopita ikisema
wapo baadhi ya watumishi wa umma waliokua
wakilipwa takribani TZS Mil.40 kwa mwezi.
Katika hatua nyingine Mafuru alisema pia kuwa
hakuna kosa lolote kwa mashirika ya umma kuwa
na fixed account kwenye benki za biashara.
Mafuru alifafanua kitaalamu sababu ambazo
zinaweza kupelekea mashirika ya umma
kufungua fixed account kwenye benki za
kibiashara. Rais aliivunja bodi ya TRA kwa madai
kuwa ilikuwa ikiweka fedha kwenye fixed account
ktk benki za kibiashara.
Lawrence Mafuru ni mtaalamu aliyebobea na
mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya
uchumi na fedha. Amewahi kuwa mkurugenzi wa
fedha wa taasisi ya Lolos Consultant, Afisa
Mtendaji Mkuu na baadae Mkurugenzi Mtendaji
wa benki ya taifa ya biashara (NBC), Mkurugenzi
wa rasilimali na masuala ya uchumi Ikulu
(Director of Resource Mobilisation and Economic
Sectors at the President Office).
Vilevile amekuwa Rais wa Taasisi ya fedha ya
ACI Financial Marketing, na Mhasibu Mkuu wa
benki ya taifa ya biashara (NBC), kabla ya kuwa
Afisa Mtendaji mkuu wa benki hiyo. Pia amewahi
kuwa Mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa
mabenki Tanzania.
Mafuru amewahi kufanya kazi pia na benki ya
Standard Chartered kama Meneja Mauzo na
mkuu wa kitengo cha ukuzaji biashara, na kuwa
mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi katika benki ya
taifa ya uwekezaji (TIB). Pia amekuwa mjumbe
wa bodi ya wakurugenzi wa taasisi ya fedha ya
Kwanza Financial Services Limited. Kwa sasa
Mafuru ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Benki ya CRDB.
Ana stashahada ya juu ya masuala ya kibenki
kutoka chuo cha usimamizi wa fedha (IFM),
Shahada ya Uzamili ya usimamizi wa biashara
(MBA) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, na
cheti cha utambuzi kinachotolewa kwa
wataalamu waliobobea kwenye masuala ya
kibenki kutoka The Chartered Institute of
Banking, London.
Unadhali kutumbuliwa kwa Mafuru kutoka Hazina
kuna uhusiano wowote na taarifa alizotoa kwenye
vyombo vya habari hivi karibuni?? Nini maoni
yako?

0 comments :

Post a Comment

Back To Top