Donard Trump ameshindwa kutamka kwa ufasaha neno Tanzania na hivi ndivo alivotamka.soma zaid
Mgombea urais wa chama cha Republican
Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya
kuonekana akiboronga akitamka Tanzania
wakati wa kutoa hotuba.
Bw Trump alikuwa akizungumzia mashambulio ya
kigaidi yaliyotekelezwa katika mabalozi ya
Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998
wakati wa kuzungumzia sera yake ya kigeni.
Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika
akitamka ‘Tan-zay-nia’.
Mashambulio hayo yalitekelezwa na mtandao wa
kigaidi wa al-Qaeda.
Msemaji wa ikulu ya White House pia alimcheka
Bw Trump alipoulizwa kuhusu vile
mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York
alivyotamka jina Tanzania.
“Kweli, yamkini jinsi ya kutamka huwa
haijaelezwa kwenye kifaa cha kuonesha
maandishi ya hotuba,” alieleza afisa wa habari
wa ikulu Bw Josh Earnest.
Video: Trump akitamka Tanzania
Trump atangaza sera zake za nje
Wakati wa hotuba hiyo, alizungumzia pia kuhusu
kundi la Islamic State ambalo kwa sasa limeanza
kunawiri nchini Libya. Kundi hilo hujulikana pia
kama Isis.
“Na sasa Isis wanapata mamilioni na mamilioni
ya dola kila wiki kwa kuuza mafuta ya Libya. Na
wajua? Huwa hatuwawekei vikwazo vya kutouza,
hatuwaangushiwi mabomu, hatufanyi lolote,”
alisema.
“Ni kana kwamba nchi yetu haifahamu
yanayofanyika, jambo ambalo huenda likawa
kweli.”
Kwenye hotuba yake, Bw Trump alikosoa sera za
kigeni za Rais Barack Obama.
Lakini Bw Earnest alipuuzilia mbali madai ya Bw
Trump ambaye kwa sasa anaongoza miongoni
mwa wagombea wanaotaka kupeperusha bendera
ya chama cha Republican.
0 comments :
Post a Comment