Haya ni mambo makuu 20 anayoyaamini Donard Trump.soma zaid
1. Waarabu-Wamarekani jimbo la New Jersey
walishangilia shambulio la Septemba 11, 2001
liliotekelezwa. Hakuna habari za kuthibitisha
haya.
2. Kunafaa kuwa na mfumo wa kufuatilia misikiti
Marekani kama njia ya kukabiliana na ugaidi.
3. Marekani inafaa kutumia njia kali za kuhoji
washukiwa katika vita dhidi ya Islamic State.
4. Trump amesema akiwa rais anaweza
kuwaangamiza Islamic State kwa mabomu na pia
kuwazuia kupata mafuta.
5. Kuundwe mfumo rahisi wa ulipaji ushuru, watu
wanaolipwa chini ya $25,000 (£16,524) wasiwe
wakilipa ushuru wa mapato.
6. Watu wenye hazina za uwekezaji ng’ambo
hawalipi ushuru wa kutosha. Lakini baadaye
alibadilika na kusema watapunguziwa ushuru
sawa na watu wa pato la wastani.
7. Anataka kujenga ukuta mpaka wa Marekani na
Mexico kuzuia wahamiaji kutoka Mexico.
8. Anataka kuwafurusha wahamiaji wote 11
milioni ambao waliingia Marekani kwa njia
haramu.
9. Yeye na Vladmir Putin wanaweza “kusikizana
vyema”.
10. Ili kuzuia visa vya watu kupigwa risasi
Marekani, nchi hiyo inafaa kuwekeza katika afya
ya akili.
11. Uchina inafaa kuchukuliwa hatua kali katika
masuala kadha ili kuhakikisha usawa wa
kibiashara kati yake na Marekani.
12. Kundi la The Black Lives Matter ambalo
hutetea haki za watu Weusi Marekani ni hatari.
13. Takwimu za sasa za Marekani ni za
kupotosha. Anasema ukosefu wa ajira umefikia
20% kinyume na takwimu rasmi zinazoonyesha ni
5.1%.
14. Utajiri wake ni $10bn.
15. Mfumo wa kutoa huduma za afya kwa
wanajeshi wa zamani unafaa kufanyiwa
mabadiliko makubwa.
16. Mpango wa Obamacare ambao ulilenga
kuongeza idadi ya Wamarekani wanaopata bima
ya afya ni “mkasa”.
17. Mabadiliko ya tabia nchi ni hali ya kawaida tu
ya hewa.
18. Ulimwengu ungekuwa pahala pema pa kuishi
kama Saddam Hussein na Muammar Gaddhafi
wangekuwa bado madalakani.
19. Angewarejesha makwao wahamiaji kutoka
Syria wanaotafuta hifadhi Marekani
.
harusi ya wapenzi wa jinsia moja, hakufaa kazi
hiyo.
20. Yeye ni “mtu mzuri sana” na anataka sana
kurejesha hadhi ya Marekani.
0 comments :
Post a Comment