Harusi yavunjika baada ya kugundulika bwana harusi alishawahikufunga ndoa na mwanamke mwingine.soma zaid
Weekend hii siku ya Jumamosi mkoani Arusha
wakati ndoa ikifungwa katika kanisa la Kiinjili la
Kilutheri ‘KKKT’, Usharika wa Usa River, wilayani
Arumeru ziliibuka vurugu baada ya pande mbili
zilizokuwa zikivutana upande mmoja ukidai
bwana harusi anafunga ndoa ya pili na Bibi
harusi aitwaye Agnes Kaaya.
Ndoa hiyo iliyokuwa ikifungwa majira ya mchana
iliingia dosari baada mwanamke aliyejulikana kwa
jina la Aneth Kimaro akiwa na kundi na watu
mbalimbali wakiwemo watoto wake kudai kuwa
Bwana Harusi ni mume wake wa ndoa.
Vurugu iliendelea kwa saa mbili zaidi kuanzia saa
nane hadi za kumi jioni huku waumini wa pande
zote mbili wakirushiana maneno makali mpaka
polisi wa kutuliza ghasia kituo cha usa river
kuingilia kati na kuwakamata kundi lililovamia
kanisani hapo akiwemo mke wa zamani, Aneth
Kimaro ambao kwa pamoja wanashikiliwa na
polisi wa kituo cha polisi Usa river.
Akizungumzia tukio hilo Bwana harusi, Ngarame
Meena alikiri kumtambua Aneth Kimaro kama
mke wake wa ndoa lakini alisema waliaachana
kutokana na ndoa yao kutawaliwa na migogoro
mikubwa na yeye kuamua kukimbilia mahakamani
kuiomba mahakama ivunje ndoa hiyo ambayo
ilifungwa mwaka 1993.
AAidha ameongeza kuwa ndoa yake ilikumbwa na
migogoro mingi tangu mwaka 1996 na
ameshasuluhisha maeneo mbalimbali ikiwemo
kwa mkuu wa wilaya ya Arusha, Meru na baraza
la kata la ndoa bila mafanikio baadaye aliamua
kwenda mahakamani kuomba ndoa hiyo ivujwe
na ilipofika November 27 2015 mahakama ilitoa
hati ya kuvunja ndoa hiyo na yeye kuwa huru
kufunga ndoa nyingine.
0 comments :
Post a Comment