ICC kuishitaki Marekani?
Ripoti ya awali ya mahakama ya kimataifa ya
uhalifu wa kivita ICC, imebaini kwamba jeshi la
Marekani na shirika la ujasusi CIA, huenda
zilitekeleza makosa ya jinai dhidi ya binadamu
nchini Afghanistan.
Ripoti hiyo, iliyotolewa na mwendesha mshataka
wa mahakama hiyo Fatou Besouda, inasema
kwamba ushahidi wa wafungwa 100 umebaini
kwamba walinyanyaswa na kudhulumiwa, huku
wengine wakibakwa.
Ripoti hiyo inasema visa vingi vilitokea mwaka
2003 na 2004, japo kuna visa vimeripotiwa
miaka 2 ilopita.
Uhalifu sawa na huo unasemekana
umetekelezwa katika vizuizi vya siri
vinavyosiomamiwa na CIA nchini Poland,
Romania, na Lithuania.
0 comments :
Post a Comment