Maajabu tena# Mwezi mkubwa zaid kuonekana Dunian.soma zaid
Watazamaji wa anga wanajiandaa kuuona mwezi
mkubwa zaidi wakati ambapo utakaribia dunia
tangu 1948.
Uingereza itakuwa na fursa nzuri kuuona mwezi
huo siku ya Jumatatu jioni,licha ya kuwa
utakaribia dunia mwendo wa saa tano na dakika
21 muda wa GMT ambapo utakuwa umbali wa
kilomita 356,509.
Wachunguzi watauona mwezi huo kuwa mkubwa
zaidi kwa asilimia 7 ukilinganishwa na mwezi wa
kawaida na kung'aa zaidi ya asilimia 15, licha ya
kwamba macho ya binaadamu yanaweza
kupambanua tofauti hiyo.
Huku mwezi huo ukitarajiwa kutokaribia dunia
hadi tarehe 25 mwezi Novemva 2034, idara ya
maswala ya hewa nchini Uingereza imesema
kuwa kutakuwa na mawingu mazito wakati
mwezi huo utakapokaribia.
Huku mwezi ukizunguka dunia,kuna tofauti ya
mwangaza unaotolewa na jua.Ni wakati huo
ambapo mwezi wote humulikwa na mwangaza
huo na kutoa mwezi mkubwa zaidi.
0 comments :
Post a Comment