Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, November 17, 2016

Mrema ameilalamikia jeshi la magereza mkoani Dodoma.soma zaid


Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Augustino
Lyatonga Mrema amelilalamikia Jeshi la
Magereza mkoa wa Dodoma kwa kukwamisha
mikakati yake ya kunusuru na kupunguza
msongamano wa wafungwa Magerezani ili
kuepuka magonjwa ya mlipuko na kusaidia
wafungwa wagonjwa, wazee, na wanawake
ambao hawajiwezi kutoka Magerezani.
Amesema hayo mapema hii leo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam, Mrema amesema amezuiwa kuendelea
na mpango huo bila ya kupewa sababu za msingi
na kutanabaisha kuwa kuna wafungwa ambao
teyari wamesha lipiwa parole zao na wanatakiwa
watoke lakini bado wako gerezani.
“Nilipata wafadhili kama Mchungaji Getrude
Lwakatare kajitolea tuwasaidie wale wafungwa
waliokosa dhamana tuwasaidie kuwalipia ili
watoke magerezani, lakini kuna watu
wamejitokeza wanasema eti tunatetea wahalifu
hii sio kweli hata kidogo”alisema Mrema.
Aidha, amemuomba Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa kuliamuru Jeshi la Magereza mkoa wa
Dodoma liruhusu zoezi hilo liendelee ili kuisaidia
Serikali kuondokana na mzigo mkubwa wa
kuhudumia wafungwa wenye makosa madogo
madogo na wagonjwa pamoja na wazee.
Mrema ameongeza kuwa kuna watu
wanamzunguka ili kukwamisha jithada zake za
kuisaidia Serikali na kutoa ombi kwa Waziri Mkuu
kuwachukulia hatua kali za kinidhamu viongozi
wote wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma
wanaokwamisha mpango huo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top