January 21, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, November 17, 2016

Mwanamke afa akiombewa kwa'Nabii' mkoani Arusha.soma zaid


MWANAMKE mkazi wa Unga-Limited jijini hapa,
Lightness Kivuyo ameripotiwa kufa wakati
akifanyiwa maombi nyumbani kwa mchungaji
aliyejulikana kama ‘Nabii Rajabu’ eneo la Kwa-
Mrombo pia jijini hapa.
Kwa mujibu wa dada wa marehemu, Juliana
Kivuyo, Lightness alikuwa amesindikizwa
nyumbani kwa nabii huyo nyakati za usiku na
mumewe aliyemtambulisha kama Shafii
Mohammed na kwamba wakati akifanyiwa ibada
ya maombi, alianguka na kufariki miguuni mwa
‘Mtume,’ huyo.
“Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema,
huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali
mbaya kule kwenye maombi,” alisema Juliana na
kuongeza kuwa alitoka mbio kwenda Kwa-
Mrombo nyumbani kwa Nabii Rajab na kumkuta
dada yake amelazwa kwenye kochi, akiwa bila
nguo isipokuwa tu khanga alizofunikwa nazo.
Nabii huyo pia anadaiwa kumnyoa nywele zote
pamoja na nyusi za macho wakati akimfanyia
‘huduma,’ hiyo.
Polisi jijini hapa wamethibitisha tukio hilo
wakiongeza kuwa tayari watu wawili
wamekamatwa kutokana na kifo hicho cha
‘maombi tatanishi.’
Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles
Mkumbo ameongeza kuwa atatoa taarifa kamili
mara baada ya kikao chake na Mkuu wa Mkoa.
Mganga Mkuu katika Hospitali ya Mkoa wa
Arusha ya Mount Meru, Jacqueline Uriwo amekiri
kupokea mwili wa marehemu, lakini akasema,
“Kwanza walijaribu kutudanganya kuwa huyo
mama alikuwa hai na kwamba aliletwa kwa ajili
ya matibabu, lakini tukagundua kuwa
walichokileta ni mwili mfu, hivyo tukampeleka
kwenye chumba cha kuhifadhi maiti!.”
Mkurugenzi wa Huduma ya Mazishi katika
hospitali hiyo ya mkoa, Dk Francis Coster
alisema mwili ulipelekwa hapo na mume wa
marehemu ambaye alisisitiza kuwa mkewe
hajafa, bali kazimia tu na kwamba mara nyingi
huzimia kwa saa nyingi.
Dk Coster aliongeza kuwa ilibidi na wao
wasiweke mwili kwenye jokofu na kuulaza
kwenye machela kwa saa sita na ndipo
wakaamua kuuweka kwenye droo za maiti, kwani
ilikuwa wazi sasa kwamba asingeamka tena
asilani.
Waganga hospitalini hapo wamekiri kuwa mwili
wa marehemu uliletwa hospitalini hapo ukiwa
umenyolewa upara, lakini ukiwa na mikwaruzo
pamoja na uvimbe hususan maeneo ya mikono
na kifua.
Baba mkubwa wa marehemu, Ally Kivuyo ambaye
ndiye mlezi wa Lightness, alisema mume wa
marehemu alimtaarifu juu ya kifo hicho na
kuongeza; “Lakini baadaye nikaletewa taarifa
nyingine kuwa Lightness kumbe alikufa wakati
akifanyiwa maombi au vitu vingine, nyumbani kwa
mtu anayeitwa ‘Nabii Rajabu,’ hapo basi ikabidi
niwataarifu polisi ambao walikuja kumkamata
mumewe pamoja na huyo anayejiita nabii au
mtabiri.”chanzo habar leo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top