Polisi imekabidhiwa majina 30 ya wanaodaiwa kuwa ni matapeli wa Aridh.soma zaid
Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekabidhi
polisi majina ya watu 30 wanaodaiwa kuwa
matapeli wa ardhi ili washughulikiwe.
Waziri huyo amelidokeza gazeti hili kuwa
amekabidhi majina hayo kwa Kamanda wa Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ambaye
alithibitisha kupokea majina hayo na kwamba
tayari yameshafunguliwa majalada kwa ajili ya
upelelezi.
“Ni mapema mno kuzungumzia jambo hili, kwa
sababu lipo kwa wapelelezi. Ni kweli majina haya
tumeyapokea na tayari majalada yamefunguliwa,”
alisema.
0 comments :
Post a Comment