Polisi asakwa akidaiwa kumpiga polisi mwenzake hadi kufa.
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga linamsaka askari
wa jeshi hilo, Michael Komba kwa tuhuma za
kumpiga askari mwenzake wa kike hadi
kumsababishia kifo.
Taarifa zilizothibitishwa na Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga, David Mngambugha,
zinamtaja marehemu kuwa ni polisi Elizabeth
Stefano wa Kituo cha Polisi Kati, Chumbageni,
jijini Tanga.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 9:00 usiku wa
kuamkia juzi, eneo la Sahare jijini Tanga ambako
ni nyumbani kwa marehemu.
Wakizungumza na Nipashe kwa sharti la
kutoandikwa majina yao gazetini, baadhi ya
majirani walidai kuwa chanzo cha ugomvi huo
kinadhaniwa kuwa ni wivu wa mapenzi, wakidai
kwamba Kombo alikuwa akimtuhumu Elizabeth
kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao.
Source: Nipashe
0 comments :
Post a Comment