Al -Shabab wamedai kuwaua wanajeshi zaid ya 50 mpakani mwa somali na kenya.soma zaid
Kundi la al-Shabab nchini Somalia
limesema wapiganaji wake
wameshambulia kambi ya wanajeshi wa
Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha
Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.
Wapiganaji hao wanadai kuwaua
wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo
katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa
Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na
Kenya.
"Mujahideen (wapiganaji) wawili
walivurumisha magari yaliyokuwa na
mabomu na kuyalipua kwenye lango la
kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya
wapiganaji wengine kuingia. Baada ya
makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka
kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab
Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia
shirika la habari la Reuters.
Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua
wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari
na silaha za wanajeshi hao, taarifa
ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya
amekanusha.
Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters:
"Ni uongo. Operesheni ya kijeshi
inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa."
Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya
serikali ya inayoungwa mkono na mataifa
ya magharibi na jamii ya kimataifa.
0 comments :
Post a Comment