Breaking News
Loading...

Advert

Friday, January 27, 2017

Moto wasababisha maafa na watu 6,000 wakimbia makazi.soma zaid

Watu 6,000 wameyakimbia makazi yao na
mmoja amefariki dunia baada ya moto
mkubwa kuteketeza sehemu ya Mji wa
Santa Olga nchini Chile.
Mataifa yameanza kutuma wazima moto
nchini Chile kusaidia taifa hilo kukabiliana
na moto mbaya zaidi katika historia ya
taifa hilo.
Urusi imetuma ndege yenye uwezo wa
kubeba tani kadha za maji kujaribu
kusaidia kuzima moto huo wa nyika.
Moto huo umeenea kwa kasi sana
maeneo ya kati ya Chile, ambapo
unasaidiwa na upepo mkali, kiwango cha
juu cha joto na hali kwamba maeneo
hayo yamekabiliwa na kiangazi kwa muda.
Mji Santa Olga, unaopatikana kilomita 240
kusini mwa Santiago umeharibiwa kabisa
na moto huo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top