Mchungaji afikishwa mahakamani kwa kumbaka mwanaye wilayani Hai.soma zaid
Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste Church
Tanzania (FPCT) Tawi la Gezaulole wilayani Hai,
Emanueli Mwikizu (42) amefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Hai kwa tuhuma za
kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 7.
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo
mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Anold
Kirekiano mwendesha mashtaka wa polisi, Elisha
Moleli amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa
la kuzini akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo
mnamo Januari 17 mwaka huu nyumbani kwake
mtaa wa Gezaulo majira ya saa 3:30 asubuhi kwa
kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia
maumivu makali sehemu zake za siri.
Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo ambapo
hakimu anayesikiliza kesi hiyo aliharisha hadi
Februari 9 mwaka huu itakapotajwa tena na
mtuhumiwa yupo rumande baada ya kushindwa
masharti ya dhamana.
0 comments :
Post a Comment