Asikari ajinyonga wilayani Igunga mkoan Tabora.soma zaid
Askari aliyejiua ametambulika kwa jina la G.4185
PC Geofrey Mwenda (32 ) ambaye inadaiwa
hawara yake mpya ndio chanzo cha kuchukua
maamuzi ya kutoa uhai wake.
By Robert Kakwesi, Mwananchi
Tabora. Askari aliyekuwa akifanya kazi kituo
kidogo cha polisi tarafa ya Igurubi wilayani
Igunga mkoani Tabora, amejiua kwa kujinyonga
kwa kutumia shuka kutokana na kinachodaiwa
kuwa ni wivu wa mapenzi.
Askari aliyejiua ametambulika kwa jina la G.4185
PC Geofrey Mwenda (32 ) ambaye inadaiwa
hawara yake mpya ndio chanzo cha kuchukua
maamuzi ya kutoa uhai wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa
alisema tukio hilo limetokea juzi saa tatu usiku.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Issa alieleza kuwa
askari huyo baada ya mke wake kusafiri, aliamua
kuchukua uamuzi ya kuwa na mpenzi wa nje.
Alieleza askari huyo baadaye alikuja kugundua
mpenzi wake ambaye hakuweza kumtaja jina
lake, kuwa alikuwa na mwanaume mwingine
mbali ya askari huyo.
Kutokana na ugunduzi huo ambao ulimfanya
askari huyo achukie ndio alipoamua kujiua kwa
kujinyonga kwa kutumia shuka na kujining’iniza
kwenye mti.chanzo mwanachi
0 comments :
Post a Comment