Kisarawe II kupata umeme wa uhakika.soma zaid
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo kuhakikisha eneo la Kisarawe II
linakuwa na umeme wa uhakika ili kuwezesha
viwanda na wananchi wa eneo hilo kupata
nishati hiyo.
Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumanne, Januari 3,
2017) wakati alipotembelea kiwanda cha
Milkcom kinachozalisha bidhaa za maziwa na
kiwanda cha Watercom kinachozalisha maji
vilivyoko katika kata ya Kisarawe II wilayani
Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.
“Waziri wa Nishati ahakikishe eneo hili linapata
umeme wa uhakika ili kuviwezesha viwanda hivi
kufanyakazi vizuri jambo litakaloongeza
uzalishaji. Pia wananchi wanaoishi katika
maeneo haya nao watanufaika na upatikanaji wa
nishati hiyo,” alisema.
Waziri Mkuu alisema amefarijika na jitihada za
muwekezaji huyo za kuunga mkono mkakati wa
Serikali ya awamu ya Tano wa kuifanya
Tanzania kujenga uchumi wa viwanda
utakaoliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kipato
cha kati ifikapo mwaka 2025.
Awali, Msemaji wa Viwanda hivyo, Aboubakar
Faraj akisoma taarifa ya viwanda hivyo kwa
Waziri Mkuu alisema moja ya changamoto
zinazowakabili ni pamoja na upatikanaji wa
umeme wa uhakika jambo linasababisha
kupanda kwa gharama za uzalishaji.
“Punde umeme unapokatika tunalazimika
kutumia majenereta kwa muda mrefu. Hii
husababisha ongezeko la gharama za uzalishaji
ambazo huumiza kiwanda kwa sababu
haiwezekani kumtwisha mzigo huu mlaji,”
alisema.
Faraji alisema changamoto nyingine ni
miundombinu ya barabara ambayo usababisha
wateja wengi kushindwa kufika kwenye viwanda
hivyo kwa urahisi, hivyo aliiomba Serikali
kuwatatulia kero hilo.
Aliongeza kuwa kwa sasa viwanda hivyo
vimeajiri watu zaidi ya 1,800, ambapo alisema
endapo Serikali itawahakikishia upatikanaji wa
umeme na barabara wataongeza ajira kwa
asilimia 25 ifikapo mwaka 2018.
Mapema Waziri Mkuu alizindua wodi ya wazazi
katika Zahanati ya Kisarawe II iliyojengwa kwa
ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Oilcom. Wodi
hiyo yenye vyumba vitatu itawapunguzia
akinamama kusafiri umbali mrefu kutuata
huduma hiyo.
0 comments :
Post a Comment