Breaking News
Loading...

Advert

Monday, January 23, 2017

Maafa yatokea nchini marekani watu 18 wafariki kutokana na kimbunga kikali.soma zaid

Watu zaidi ya 18 wamefariki kutokana na
kimbunga kikali na hali mbaya ya hewa
kusini mwa Marekani, maafisa wa uokoaji
wamesema.
Watu wengi wamejeruhiwa. Maeneo
yaliyoathiriwa zaidi ni majimbo ya Georgia
na Mississippi.
Gavana wa Nathan Deal ametangaza hali
ya tahadhari katika wilaya saba kusini na
katikati mwa Georgia ambapo watu 14
wamefariki.
Watu wanne waliuawa na vimbunga
Mississippi siku ya Jumamosi.
Bado kuna hatari ya kimbunga kupiga
maeneo ya kusini mwa Florida, idara ya
taifa ya hali ya hewa imeonya.
Idara ya huduma za dharura ya Georgia
imesema watu 14 walifariki katika wilaya
za Cook, Brooks, Dougherty na Berrien
katika jimbo la Georgia.
Nyumba nyingi zimebomolewa katika
wilaya ya Cook.
Rais wa Marekani Donald Trump
amesema amewasiliana na Gavana Deal
na kumpa salamu za rambirambi
kutokana na vifo vilivyotokea.
Kusini mwa Mississippi, watu wanne
walifariki kutokana na kimbunga ambacho
kilikuwa na upepo uliokuwa unavuma kwa
kasi ya 218 km/h (136 mph).
Watu zaidi 50 walijeruhiwa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top