February 19, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, January 22, 2017

Akutwa amekufa akiwa na vibuyu 5,kuku mweupe.soma zaid


BIBI mwenye umri wa miaka 60 amekutwa
amekufa mkoani Tabora huku amevaa nguo
nyeusi aina ya kaniki, akiwa na vibuyu vitano na
kuku mweupe, katika mazingira yanayoashiria
kushiriki vitendo vya kishirikina.
Aidha, mwili wa mtu mwingine umekutwa
pembeni ya mti aliokuwa akichimba dawa.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis
Selemani iliwataja waliokutwa wamekufa kuwa ni
Nsoma Dotto (60) mkazi wa Kijiji cha Zugimlole
Wilaya ya Kaliua na Mayara Marashi (50) ambaye
ni mkazi wa Igunga.
Kamanda Selemani alisema Nsoma alikutwa
akiwa amekufa umbali wa mita 200 kutoka
nyumbani kwake juzi.
Alisema bibi huyo alikutwa amevaa nguo nyeusi
aina ya kaniki akiwa na vibuyu vitano huku
pembeni yake kukiwa na kuku mweupe.
Uchunguzi wa awali wa jeshi hilo, unaonesha
kuwa huenda ni imani za kishirikina.
Aidha, alisema Marashi ambaye ni mkazi wa Kijiji
cha Mwakapinga, Kata ya Nanga, aliyekuwa
mganga wa kienyeji, mwili wake uliokotwa
Januari 16, mwaka huu ukiwa umeanza
kuharibika.
Kwa mujibu wa Kamanda Selemani, mganga huyo
wa kienyeji aliondoka nyumbani kwake Januari 8,
mwaka huu kwenda porini kuchimba dawa, lakini
hakurudi kijijini hadi maiti yake ilipookotwa akiwa
amekufa.
Alisema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo
hicho. Aliwaomba wananchi wanaoenda porini
kwa ajili ya shughuli zozote zile, wawe wanatoa
taarifa kwa ndugu zao ili iwe rahisi tatizo
linapotokea.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top