Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, January 25, 2017

Mbunge wa morogoro mjini mh.Abood amemwaga neema ya mamilioni kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.soma zaid.

MBUNGE wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood
(CCM), amekabidhi Sh milioni 48 kwa ajili ya
kulipia ada wanafunzi wa elimu ya juu, shule za
sekondari na shule za msingi waliopo ndani ya
Manispaa ya Morogoro kwa kipindi cha Januari
mwaka huu.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana mjini hapa
mbele ya wazazi, ambapo Abood alisema suala la
elimu linapaswa kupewa kipaumbele kwa kuunga
mkono jitihada zinazofanywa na wadau kwa
kushirikiana na Serikali.
Alisema kuwa hakuna haja ya mzazi na mlezi
kuacha ama kushindwa kumpeleka mwanae shule
wakati Serikali iliondoa mfumo wa malipo kwa
wanafunzi wa shule za msingi na kuacha
majukumu ya kununua sare, mahitaji mengine
kwa wazazi na walezi.
“Mimi kama mzazi nimeamua kujinyima na
familia yangu tuwapokee baadhi ya wazazi
majukumu, maana hawa ni watoto na wengijne ni
vijana wangu wanastahili kupata elimu bora,
hakuna urithi mzuri kama kumpa mtoto elimu,”
alisema Abood.
Alisema fedha alizotoa ni kutokana na vyanzo
vyake vya mapato huku akiwa amedhamiria
kuimarisha elimu hasa kwa watoto, vijana wa
jimbo lake kwa kuwasaidia wazazi sehemu ya
majukumu yao.
Mbali na hilo mbunge huyo amekabidhi mbao
zenye thamani ya Sh milioni 9.8 kwa ajili ya
ukarabati wa Shule ya Msingi Kauzeni
iliyoezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na
upepo mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumzia hatua hiyo mkazi wa Morogoro,
Said Mkwinda alisifu jitihada zinazofanywa na
mbunge huyo katika kuboresha sekta ya elimu
pamoja na huduma mbalimbali jimboni humo.
“Hakuna mtu anayefika katika ofisi ya mbunge
kuomba msaada ana kosa, Abood anatoa msaada
kwa watu wote bila itikadi ya chama, dini wala
kabila,huyu ndiyo kiongozi watu anapaswa
kuungwa mkono katika kazi yake ya ubunge,”
alisema.chanzo mtanzania

0 comments :

Post a Comment

Back To Top