January 21, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, January 25, 2017

Mbunge kubenea afutiwa kesi yake lakini akamatwa tena na polisi.soma zaid

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu imeyaondoa mashtaka ya
uchochezi yaliyokuwa yakimkabili Mbunge
wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (46).
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri,
leo ameyaondoa mashtaka hayo
mahakamani hapo kwa sababu hati ya
mashtaka ilikuwa na utata na aiendani na
kifungu cha 132 cha Sheria ya Mwenendo
wa Makosa ya Jinai (CPA).
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri
alisema kifungu hicho cha sheria kinataka
kosa lielezwe kwa uwazi ' kinaga ubaga'.
Alisema katika kesi ya uchochezi
iliyokuwa ikimkabili Kubenea ya
kusambaza habari ya uongo yenye kichwa
cha habari 'yuko wapi atakayeiokoa
Zanzibar' ambayo ingeweza kuleta
uvunjifu wa amani, Hakimu Mashauri
alisema maneno hayo pekee kisheria siyo
kosa.
Akiendelea kutoa uamuzi huo, Hakimu
Mashauri alisema upande wa mashtaka
ulishindwa kueleza maneno yenyewe hasa
ya uchochezi yenye lengo la uvunjifu wa
amani.
Hivyo, Hakimu Mashauri aliiondoa kesi
hiyo mahakamani hapo na mshtakiwa
akaachiwa huru na kwamba upande wa
mashtaka unaweza kumshtaki upya.
Hata hivyo baada ya Kubenea kuachiwa
huru alikamatwa na kupelekwa polisi kati
na baadaye akaachiwa kwa dhamana.chanzo jamii forums

0 comments :

Post a Comment

Back To Top