Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, May 7, 2017

Makamu wa Rais mhe.Samia Suluhu Hassan amewasili mkoabi Arusha jion hii.soma zaid

KutokaArusha: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan amewasili mjini Arusha jioni hii ambapo
hapo kesho ataongoza wananchi wa mkoa wa
Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya
wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva
Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini
Arusha waliopata ajali jana tarehe 06-May-2017
katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani
Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo
wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini
kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema
baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia
na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia
wilayani Karatu.
Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao
itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hapo
kesho.
Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake
wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mhe Mrisho Gambo (@mrisho_gambo) pamoja na
Viongozi wa wengine wa mkoa huo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top