Benku kuu( BOT) imepiga marufuku mchezo wa upatu ujulikanao kama D9 CLUB.soma zaid
Malisa GJ
Benki kuu ya Tanzania (BOT) imepiga marufuku
mchezo wa upatu ujulikanao kama D9. Taarifa
iliyotolewa na BOT kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Masoko ya mitaji na dhamana (CMSA)
inasema mchezo huo ni haramu na ni kinyume na
sheria ya makosa ya jinai sura ya 16. Hii ni
kusema kuanzia sasa kile kilichoitwa D9
kimekufa rasmi. Mtu yeyote atakayeonekana
kujihusisha na mchezo huo atachululiwa hatua za
kisheria.
Nimekumbuka nilivyoshawishiwa kujiunga kwenye
mchezo huo kwa kigezo cha kupata hela
"chapchap". Sikushawishika kabisa maana najua
principle ya kupata hela ni lazima uitolee jasho.
Katika ulimwengu huu wa "kibepari" hakuna pesa
inayopatikana bila kufanya kazi.
Bahati mbaya kuna watu waliajiingiza kwenye
mchezo huu kwa kushawishiwa na watu
wanaowaamini. Wengine wakajisajili wao na
familia zao. Mtu kajisajili yeye, mke na watoto.
Kila mmoja kalipa dola 2000+, akitegemea
kuvuna dola 170 kila wiki. Leo mchezo huo
unapigwa marufuku halafu alikua hajavuna hata
mara moja. What a mess.!
Ni vizuri tukawa makini na hizi biashara za
mtandaoni. Usije kuinvest pesa yako bila kupata
taarifa sahihi juu ya biashara husika.
Mnakumbuka DECI?? Nayo ilikua hivihivi. Polen.chanzo Malisa GJ
0 comments :
Post a Comment