Mbunge Willian Ngeleja atoa yamoyini baada ya ripoti ya mchanga wa madini.soma zaid
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William
Ngeleja amesema maisha hayana budi
kuendelea.
Kwa ufupi
Ngeleja ameyasema hayo leo Alhamisi, wakati
akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali
baada ya Mbunge wa Mbozi (Chadema),
Paschal Haonga kuomba taarifa ya mbunge
huyo wa Sengerema kutajwa kuhusika kulitia
Taifa hasara kutokana na mapato ya madini.
By Julius Mnganga, Mnganga jmathias@
mwananchi.co.tz
Dodoma. Baada ya kutajwa miongoni mwa
wanaotakiwa kuchunguzwa kutokana na sakata la
mchanga wa madini, aliyekuwa Waziri wa Nishati
na Madini, William Ngeleja amesema maisha
hayana budi kuendelea.
Ngeleja ameyasema hayo leo Alhamisi, wakati
akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali baada
ya Mbunge wa Mbozi (Chadema), Paschal
Haonga kuomba taarifa ya mbunge huyo wa
Sengerema kutajwa kuhusika kulitia Taifa hasara
kutokana na mapato ya madini.
Ingawa Mwenyekiti wa Kikao, Mussa Azzan
Zungu ameikataa taarifa hiyo, lakini Ngeleja
amesema:
"Kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia, maisha
yanaendelea."
Baada ya maneno hayo machache aliendelea
kutoa mchango wake.
Ngeleja na baadhi ya mawaziri wa zamani
wametajwa kuhusika kwa namna moja au
nyingine katika sakata la usafirishaji wa mchanga
wa madini na mikataba tata ya madini nchini
inayotajwa kulipotezea Taifa zaidi ya Sh100
trilioni.
0 comments :
Post a Comment