Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 15, 2017

Gari aina ya fusoyenye namba 880 EF imepata ajali katika daraja.soma zaid

Gari aina ya fuso yenye namba Z 880 EF
imepata ajali katika daraja la kitope wilaya ya
kaskazini B baada ya kufeli break kulikopelekea
kuacha njia na kutumbukia katika daraja la hilo.
Tukio hilo limetokea jana juni 13, 2017 majira ya
saa nne na dakika hamsini asubuhi, wakati gari
hiyo ilipokua ikitokea kazole na kuelekea mto
mchanga.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa
wa kaskazini unguja Hasina Ramadhan Taufiq
amewataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Dereva
Mbaraka Mohammed Khamis mwenye umri wa
miaka 50 mkazi wa mfenesini, mwengine ni
Emmanuel Maganga Charles miaka 26 mkazi wa
Bububu na Ali Mohammed Juma miaka 29 mkazi
wa Donge. Majeruhi wamelazwa katika hospitali
ya Mnazi mmoja na hali zao zinaendelea vizuri.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top