Chama cha mapinduzi CCM chawageuka Chenge,Ngeleja na Mhongo.soma zaid
Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kimewataka wote waliotajwa katika ripoti ya
kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya
mchanga wa madini, kutoa ushirikiano kwa
vyombo vya dola vitakavyowahoji.
Waliotajwa katika ripoti ya pili ni aliyewahi kuwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew
Chenge, waliokuwa mawaziri wa Nishati na
Madini, William Ngeleja, Profesa Sospeter
Muhongo na na Nazir Karamagi.
Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi) katika
ofisi za Lumumba, Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa CCM, Humphrey Polepole amesema ili
vyombo vya dola viweze kufanya kazi yake kwa
haraka na ufanisi, waliotajwa wanapaswa kutoa
ushirikiano.
Polepole amesema chama hicho chenye Serikali
kinaviagiza vyombo vya dola kuwahoji
waliohusika kwa haraka ili Watanzania wajue
ukweli wa yaliyotokea.
Amempongeza Rais John Magufuli kwa
kuthubutu kudai rasilimali ambazo zimekuwa
zikiibiwa.
Pia, amewataka wananchi kumuunga mkono Rais
Magufuli kwa kazi anayoifanya badala ya
kugawanyika.
0 comments :
Post a Comment