Watoto wawili wa kiuume na mmoja wa kike wamefarki jijini Mwanza.soma zaid
Watoto wawili wa kiume mmoja na wa
kike mmoja wakazi wa mtaa wa Kigoto,
wilayani Ilemela Jijini Mwanza wamefariki
dunia na wengine wawili kunusurika kifo
katika ajali ya moto iliyosababishwa na
mshumaa kushika kwenye kochi huku
mama wa watoto hao akijeruhiwa na moto
huo wakati akiwaokoa watoto wake.
Wakizungumza katika tukio majirani wa
familia hiyo wamesema kuwa moto huo
umeanza kuwaka majira ya saa nne usiku
na kwamba wamefanya jitihada za
kuwaokoa watoto hao lakini kutokana na
moto kuwaka kwa kasi wameshindwa
kuwaokoa watoto wawili
Nae baba mzazi wa watoto hao, Said
Daudi amesema kuwa wakati moto huo
unawaka katika nyumba yake hakuwepo
nyumbani hivyo alikuwepo mama yao na
alikuwa nje huku watoto wakiwa ndani
ndipo mshumaa ulishika kwenye kochi na
kusababisha madhara hayo
Kwa uapnde wa kaimu mwenyekiti wa
mtaa huo, Zakayo Yusuph amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuwomba
wananchi kuwa makini na matumizi ya
mishumaa.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo
amewataka wananchi kuzingatia matumizi
ya mishumaa kwa lengo la kuepuka na
majanga ya moto pindi wanapotumia.
chanzo; dewjiblog
0 comments :
Post a Comment