Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Wednesday, August 23, 2017
Ajali mbaya ikuhusishwa kati ya Costa na Treni Morogoro.soma zaid

Ajali mbaya ikuhusishwa kati ya Costa na Treni Morogoro.soma zaid


Ajali mbaya imetokea Mji Mpya Relini, Morogoro,
muda si mrefu kati ya treni na coaster ya
Kihonda. Coaster ilikuwa imebeba abiria wengi
wakiwemo wanafunzi.

Rais Maguful amefanya teuzi mwingine leo.soma zaid

Rais Maguful amefanya teuzi mwingine leo.soma zaid

Wednesday, August 16, 2017
Mzee Majuto ametangaza rasimi kustaafu kuigiza ili kurudi kumcha Allah.soma zaid

Mzee Majuto ametangaza rasimi kustaafu kuigiza ili kurudi kumcha Allah.soma zaid

Mchekeshaji na Muigizaji maarufu wa filamu
nchini Tanzania, Alhaji Amri Athumani almaarufu
Mzee Majuto ametangaza rasmi kustaafu kazi
hiyo baada ya kuitumikia kwa zaidi ya ,miaka 30.
Mzee Majuto
Mzee Majuto amesema amechukua maamuzi
hayo baada ya kuona umri unaenda na uwingi wa
changamoto wa kazi hiyo hivyo ameamua arudi
kwenye kilimo na kumtumikia Mungu.
“Kwa sasa hivi mimi sanaa basi , nasema kwa
kweli sanaa basi labda kutokee mtu anahitaji
nimfanyie tangazo lake nikimaliza narudi
shambani kwangu nimtumikie mwenyezi Mungu
nimuombe toba kwa sababu tuliofanya ni mengi
na kuna mazuri na mabaya na mabaya ndiyo
yanayotawala kwenye maisha ya ujana kwa hiyo
tumuombe toka Mwenyezi Mungu, kwani wakati
ndiyo huu ukisema upange siku kila siku
utapanga” ,amesema Mzee Majuto kwenye
mahojiano yake na gazeti la Habari Leo.
Licha ya kustaafu Mzee Majuto ameishauri
serikali ijenge kambi nyingi za JKT ili kupunguza
idadi ya vijana wanaokaa bila kazi mitaani.

TANZIA#.Watoto mapacha waliozaliwa mkoani Morogiro wakiwa ameungana wamerifiki dunia.soma zaid

TANZIA#.Watoto mapacha waliozaliwa mkoani Morogiro wakiwa ameungana wamerifiki dunia.soma zaid


Watoto mapacha ambao walizaliwa
mkoani Morogoro wakiwa wameungana
maeneo ya tumboni wamefariki dunia ktk
Hospitali ya Taifa Muhimbili walipokuwa
wakisubiri matibabu na jaribio la
kutenganishwa.
Haikuwa rizki!
=========================
Habari za awali kuhusu watoto hao;
=========================
Watoto mapacha waliozaliwa wakiwa
wameungana mkoani Morogoro
imegundulika kuna uwezekano wa
kuwatenganisha
Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa
Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Zaituni Bokhary
alipokuwa akitoa majibu ya vipimo
vilivyochukuliwa hospitalini hapo kwa
takribani wiki nzima.
Daktari huyo amesema kuwa baada ya
kufanya vipimo, imegundulika kuna
uwezekano wa kuwatenganisha watoto
hao mapacha.
Majibu hayo yamekuja siku chache baada
ya pacha hao kupimwa vipimo vya
radiolojia ikiwemo CT Scan, MRI, X Ray
kipimo cha moyo (ECO) pamoja na vipimo
vyote vya damu.
Watoto hao waliozaliwa katika hospitali ya
Misheni ya Berega iliyopo Kanda ya
Mashariki mkoani Morogoro, Julai 21
mwaka huu wamenaza kuchukuliwa
vipimo mbalimbali vya awali kabla ya
upasuaji huo.chanzo jamii forums

Monday, August 14, 2017
no image

Kijana epuka ndoa na wanawake yenye kazi hizi.soma zaid

Mwalimu : Wengi wenu mna dhana potofu kwamba ukioa mwalimu mpo in safe side. Hawa watu akili zao zimelala fofofo. Mtu anayeridhirika na ujira wa laki 3 kwa mwezi kwa kutoa sadaka siku zake 30 kwa mwezi ni wa kumuepuka. Hana changamoto mpya katika maisha. Akirudi kazini yuko exhausted kabisa, atapata wapi muda wa kuwaza vitu vipya huku bado hajasahihisha?? Unless atakua ni mtu unayemtumia kwa sex tu, ana madhara hata kwa akili ya watoto atakaowazaa yawezekana wakawa na akili mgando pia. Askari : Hawa watu siitaji kuwaelezea sana. Acha wachukuane wao kwa wao. Kama wewe ni raia wa kawaida ukitaka kuumia moyo kwa kupigiwa oa hawa watu. Mafunzo ya kijeshi kawaida yanaharibu saikolojia yao. Kauli mbiu ya huko mafunzoni kwao ni kwamba wanawake wapo jeshini kwa ajili ya kuburudisha mjeshi wa kiume na kumpa morali. Ko kiungo chake si mali yake. Achilia mbali kukuendesha. Nurse / Wauguzi : Kama una mpango wa familia yako kustawi kiuchumi, epuka hawa watu. Kazi zao zinawa train kutoa msaada ( kazi za kujitolea ). Mioyo na akili zao hubadilika kabisa na kuwa kimsaada na kuhurumia zaidi. Hii ni mbaya sana kwa maisha ya kibiashara/kiuchumi. Ingawa the first law of being rich is giving out but kwa hawa huwa ni too much. Wema usizidi uwezo. Madactari : Kutokana na nature ya kazi zao ni vigumu mno kwa ustawi wa familia. Kama una ndoto ya kuipeleka mbali kiuchumi familia yako waepuke. Muda wao mwingi hutumika kuwaza kazi zao na kutoa huduma. Ni rare sana kumkuta dactari yuko shap nje box. Unless umuweke kwa kukuzalia na huduma za kimwili, hata hivyo unahitaji uwe mvumilivu kwelikweli muda wowote anakurupushwa kazini. Waajiriwa wa mabenki. ( Tellers & Accountants). Kuishi mtoni haimaanishi wewe ni msafi. Kuna watoto mnajidanganya hawa watu wana pesa kutokana na kazi zao. Hawa hawana tofauti na kundi la kwanza hapo juu. Moja ya wanyonywaji wanaoongoza nchini ni hawa. Mikopo ya nyumba na vigari huwasahaulisha kabisa kama wananyonywa. Ma teller wanalipwa hadi laki 4, accountants wanapewa >1m for 12 hrs a day for 30 days. Ukiamua kuoa hawa hakikisha ana kubali kuacha kibarua chake, wanakuwaga wachakarikaji at least but wakiacha. Wasaidizi maalumu wa watu binafsi : Wasemaji wa mabosi fulani, makarani wa mabosi, na wengineo. Mara nyingi huwa ni nyama za hao mabosi, Lkn unaweza kuoa kama huna wivu wa mapenzi. Mara mia ukaoa muhudumu wa hoteli. Msomi asiye na kazi : Mara mia tatu kuoa mjinga asiye na kazi kuliko hawa nyumbu wamekula pesa ya serikali alafu wanapanga foleni kusubiri kuwa watumwa wa watu. Akili yao 80% wanawaza ngono vichwani. Mjinga asiye kazi unaweza bahatika kupata mwenye mwamko akawa wa faida kwako ila kwa sababu tu hakupata mwanga akaishia kubaki iddle. USHAURI WA BURE ( option kuchukua): Kuna kazi watu wake mnawadharau mno lakini kwa kutokana na uzoefu wangu maishani it's 100 better kuwachangamkia. Wafanya biashara wadogo( haijalishi udogo wa level gani). Akili za hawa wanawake zimechamka mno. Akili iliyochamka ina faida lukuki kwa mtumiaji. Ashajua ujanja wa kuingiza mkwanja, kuoa hawa ni kuwa na advantage ya goli la ugenini. Waajiriwa wa secta binafsi department za accounts, Sells & Marketing & Project planning & Development. Akili za hawa watu huwa ziko active muda wote kutokana na nature za kazi zao. Ni faida kwako uliye na ndoto za kufika mbali kiuchumi. Ukikosa wa secta binafsi oa hata wa serikalini. Mkishawaoa baada ya muda ni vizuri watoeni huko, wafanye mambo yanayohusu familia( kiuchumi). Mnaweza kuongeza na wengineo...............................................!! Samahanini sana kwa niliowagusa.....

Mwenyekiti wa kijiji shabani(50) amefia Gesti juu ya kifua cha binti mwenye umri chini ya miaka(30)soma zaid

Mwenyekiti wa kijiji shabani(50) amefia Gesti juu ya kifua cha binti mwenye umri chini ya miaka(30)soma zaid

INASIKITISHA sana! Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkamba Kata ya Kimanzichana mkoani Pwani aliyetambuliwa kwa jina moja la shabani anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, anadaiwa kufia kifuani mwa binti mwenye umri wa chini ya miaka 30, wakiwa kwenye gesti moja iliyopo Mzinga-Mbagala jijini Dar. IJUMAA WIKIENDA LATONYWA Mara tu baada ya kujiri kwa tukio hilo lililoibua simanzi nzito, Ijumaa Wikienda ambalo huwa halilazi damu kufika eneo la tukio na kuanika kila kitu, lilitonywa na chanzo chake, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo lilifika na kuibuka na mkanda kamili wa sakata hilo. Wawili hao walidaiwa kufika kwenye gesti hiyo na kuomba huduma ya kulala kabla ya kutokea kwa tukio hilo baya. WALITOKEA KIMANZICHANA Mwenyekiti huyo alikumbwa na umauti Agosti 11, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa meneja wa gesti hiyo, Hamadi Haji, walipofika, wawili hao walichukua chumba tangu Agosti 8, mwaka huu wakitokea huko Kimanzichana. Meneja huyo aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, baada ya kulipia chumba, wawili hao walikuwa wakifika usiku kulala na mchana walikuwa wakitoka kwenda kwenye mihangaiko yao. “Sijui walikokuwa wakienda, lakini walikuwa wakirudi usiku na kujifungia chumbani. MSHANGAO “Lakini katika hali ya kushangaza leo (Ijumaa iliyopita) asubuhi, mwanamke aliyekuwa na mwenyekiti alinifuata na kuniambia mwenzake huyo hamwelewi kwa sababu ghafla alianza kumbadilikia na kukoroma kwa mlio ambao haukuwa wa kawaida. “Yule mwanamke aliniambia kiongozi huyo alikuwa na dozi fulani aliyopewa baada ya kutoka hospitalini kwa sababu hakuwa vizuri kiafya na hilo ndilo lililowaleta Dar. “Alisema alimkatalia sana wasifanye tendo la ndoa, lakini usiku mzima alikuwa akimlazimisha. “Yule mwanamke alitueleza kuwa baada ya jamaa kumbembeleza sana na kumuongezea na vishawishi vingine, mwanamke alisema alijikuta akilegeza msimamo kisha akamkubalia asije akaona labda hampendi. “Baada ya kumkubalia ndipo wakaanza kufanya yao. MUUNGURUMO WA AJABU “Aliendelea kutusimulia kuwa wakati wakiendelea kufanya yao ndipo alipoanza kumsikia mwenzake akitoa muungurumo wa ajabu huku akimng’angania kifuani. “Alitusimulia kuwa alipoona hivyo, akaanza kumshangaa, lakini ghafla alimuona akitupatupa miguu na mikono. “Alisema baada ya kuona hivyo, alijinasua na kumwangalia mwenzake kwa makini ndipo akamshuhudia akitupatupa mikono na miguu peke yake. “Yule binti alisema kila alipojaribu kumsemesha, jamaa alikuwa hawezi kujibu lolote hivyo alikaa muda fulani akijua mwenzake labda amekumbwa na jambo la kawaida na atarejea kwenye hali yake. UKIMYA WATAWALA “Alisema tofauti na matarajio yake, jamaa aliendelea kuwa kimya na hapo ndipo alipoingiwa na hofu. “Alipoona hivyo, ndiyo akaja kunigongea kwenye ofisi yangu. Mimi nikaenda naye kwenye chumba chao kiitwacho Mikumi na kumkuta jamaa amelala kwa staili ambayo hata mimi mwenyewe sikuilewa. “Ilibidi nimpigie simu mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu, aje tushirikiane kumuangalia,” alisimulia meneja wa gesti hiyo na kuongeza: “Muda mfupi baadaye, mwenyekiti aliwasili na viongozi wenzake na kuingia kwenye hicho chumba ambapo walipomuangalia jamaa, waliniambia kuwa huenda amefariki dunia. “Hapo ndipo wakapiga simu polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo baada ya kugundua jamaa alikuwa amekwishafariki dunia.” MWENYEKITI ATHIBITISHA Kufuatia sakata hilo, Ijumaa Wikienda lilifika kwenye ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mzinga A na kumkuta mwenyekiti wa mtaa huo, Chande Mpwati ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo mtaani kwake na kueleza jinsi alivyoshiriki katika kwenda kuukagua mwili wa marehemu na kumuhoji binti aliyekuwa naye. MAPENZI YA SIRI Mpwati alisema kuwa, alipomuhoji binti huyo alimwambia kwamba jamaa huyo alikuwa ni mpenzi wake wa siri kwa kuwa ana familia yake kijijini kwao, Mkamba maana mwanamke huyo naye ni mkazi wa huko hivyo walikuja Dar kwa ajili ya mwanaume huyo kutibiwa ambapo walinionesha makaratasi ya hospitalini ndipo umauti ukamfika wakiwa wanafanya mapenzi. “Mwili wake ulichukuliwa na polisi kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Temeke na yule binti alichukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi,” alisema mwenyekiti huyo. KAMANDA TEMEKE Ijumaa Wikienda lilizungumza na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Gilles Muroto ambaye alisema kuwa ishu hiyo ilikuwa haijamfikia mezani kwake, lakini aliahidi kufuatilia kwa watu walio chini yake. MAZISHI Habari zilizolifikia Ijumaa Wikienda zilieleza kuwa, kiongozi huyo alizikwa kijijini kwake, Mkamba huko Kimanzichana, Jumamosi iliyopita. Source: Global Publisher
Friday, August 11, 2017
Mama ameamua kumlipa hela mke wa mwanae ili asitoke nje ya ndoa baada ya kugundua anamsaliti mwanae.soma zaid

Mama ameamua kumlipa hela mke wa mwanae ili asitoke nje ya ndoa baada ya kugundua anamsaliti mwanae.soma zaid


Mama mmoja nchini Afrika kusini ameamua
kumlipa hela mke wa mwanae ili asitoke nje ya
ndoa. Mama huyo alifanya hayo baada ya
kugundua binti huyo (mke wa mwanae)
anamsaliti mumewe.

Mbunge wa Manyon mashariki asababisha ajali.sima zaid

Mbunge wa Manyon mashariki asababisha ajali.sima zaid


# Habari:Watu watatu wamekufa katika ajili mbili
tofauti wilayani Manyoni ,ikiwemo ya mbunge wa
Manyoni mashariki kumgonga mwanafunzi wa
darasa la kwanza na kufariki papo hapo ,na ajali
nyingine gari aina ya Hiace kuligonga lori kwa
nyuma na kusababisha vifo vya watu wawili papo
hapo.

Afsa habari wa TFF Alfred Lucas amerudishwa Dar kwa kosa la kumsalima mgimbea wa urai Tff.soma zaid

Afsa habari wa TFF Alfred Lucas amerudishwa Dar kwa kosa la kumsalima mgimbea wa urai Tff.soma zaid


HABARI MPYA: Afisa Habari wa TFF, Alfred
Lucas amerejeshwa Dar kwa kosa la kumsalimia
mgombea urais wa shirikisho hilo, Richard Shija
akidaiwa anampigia kampeni.

Back To Top