MICHEZO
BURUDANI
SIASA & JAMII KWA UJUMLA
Recent Post
Kenya:.mwendesha mashitaka mkuu inchini kenya ameamuru uchunguzi ufanyike dhisi ya tume ya kusimamia uchaguzi nchini kenya IEBC.
. Hii ni kuhusiana na makosa yaliyofanyika wakati ilipokuwa ikishughulikia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita. Bwana Keriako Tobiko ameiomba idara ya polisi pamoja na tume ya kupambana na ufisadi nchini humo, kuwasilisha kwake ripoti ya uchunguzi huo katika kipindi cha siku 21 zijazo. Pia amewaomba kuchunguza madai kuwa, maafisa wawili wakuu wa muungano wa upinzani nchini Kenya, walifaulu kudukua kompyuta za tume ya uchaguzi. Hiyo inafuatia uamuzi wa mahakama ya juu zaidi nchini Kenya kufutilia mbali uchaguzi wa Urais wa Agosti nane kwa madai kwamba kulikuwa na makosa chungu nzima, huku mahakama hiyo ikikataa kuwalaumu moja kwa moja maafisa wakuu wa tume hiyo kwa kufanya makosa. Tarehe ya Uchaguzi mwingine imetangazwa kuwa Oktoba 26.
polisi wamshilia mwanafunzi wa chuo cha IFM kwa kumiliki Bastola.soma zaid
Polisi Dar wanamshikilia mwanafunzi wa chuo cha IFM mwaka wa tatu mkazi wa Segerea anayeitwa Robson Isack Maji kwa kukutwa na bastola aina ya Beretta ikiwa na risasi 6 ndani ya magazine Polisi walipata taarifa kuna watu hukodisha silaha kwa majambazi ili wafanye uhalifu na kisha walipwe fedha, ndipo walipoanza kufuatilia na kumnasa mwanafunzi huyo , katika maelezo ya awali anadai silaha hiyo na pia angeiuza kwa shilingi milioni mbili na nusu na alikuwa ameiiba kwa baba yake anayefahamika kwa Isack Maji ambaye pia sio mmiliki halali wa silaha hiyo, amabye polisi imemkamata pia. Mshitakiwa amekiri kosa hilo na amemtaja Patrick Makai ambaye pia polisi wamemkamata kama mshirika wake kwenye kukodisha silaha kwa majambazi. Polisi mpaka sasa wanamtafuta mmiliki halali wa silaha hiyo. Polisi pia wamekamata gari ya wizi lenye usajili wa T364 DJV Noah Nyeupe huko Mbezi, Polisi wanawashikilia Mustapha Hassan Mkazi wa Kimara Mwisho Athuman Peter Ngosha mkazi wa Kivule na wamebaini watuhumiwa waliiba gari hiyo tarehe 21/09/2017 kwa mtu anayefahamika kwa jina la Shoo huko Bunju na bado wanamtafuta mtuhumiwa mmoja aliyefanikiwa kukimbia Pia polisi imewakamata watuhumiwa 203 kwa kupatikana na pombe haramu ya gongo na madawa ya kulevya aina ya bangi, lita 1,479 za gongo na mitambo 14 ya kutengeneza pombe hiyo pia vimekamatwa Pia polisi wamekamata vyombo vya usafiri kwa makosa 11,374 na kukusanya faini kiasi cha Shilingi 33,9510,000 kutokana na makosa hayo -
Tume ya uchaguzi Kenya imetangaza tare ya uchaguzi wa marudio. soma zaid
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya imetangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais, Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. "Hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wa urais katika uchaguzi huo upya. Waliopinga matokeo ya uchaguzi kortini, Bw Raila Odinga na mgombea mwenza wake Stephen Kalonzo Musyoka na mshtakiwa wa tatu Rais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Samoei Ruto, watakuwa ndio wagombea pekee," taarifa ya bw Chebukati imesema. Katika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Mahakama ya Juu iliiwekea lawama Tume ya Uchaguzi. Majaji wa tume hiyo hawakuandaa uchanguzi huo kwa viwango vilivyowekwa kwenye katiba na sheria za uchaguzi, na kwamba kulitokea kasoro nyingi sana katika mchakato wa kupeperusha matokeo. Bw Chebukati amesema tume hiyo inafanyia utathmini mifumo na taratibu zake kwa ajili ya uchaguzi huo mpya. Mwenyekiti huyo hata hivyo ametoa wito kwa Mahakama ya Juu kutoa hukumu ya kina kuhuhusu kesi iliyowasilishwa na Bw Odinga kupinga ushindi wa kenyatta ili kuiwezesha "tume kutambua maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa katika usimamizi wa uchaguzi mpya". Majaji wa mahakama ya juu waliahidi kutoa hukumu kamili kabla ya tarehe 22 mwezi huu. IEBC ilikuwa na muda wa hadi tarehe 31 Oktoba kikatiba kuandaa uchaguzi mpya. Lakini waziri wa elimu alikuwa ameomba tume hiyo kuandaa uchaguzi huo mapema ili kutovuruga mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne ambayo imepangiwa kufanyika kuanzia mwishoni mwa Oktoba.