Askali Polisi akamatwa kwa tuhuma za mauaji.soma.zaid
Jeshi la polisi wilayani Uvinza mkoani Kigoma, linamshikilia askari mmoja kati ya wawili, kwa tuhuma za kumuua kwa risasi kijana mmoja Hamis Wales mkazi wa kijiji cha Mpeta kata ya mngaza wilayani humo. Tukio hilo lilitokea polisi walipoenda nyumbani kumkamata kijana huyo baada kutokea ugomvi kati yake na mke wake, uliosababishwa na kijana huyo kuoa mke wa pili Mashuhuda wakielezea tukio hilo wanasema askari walienda kumkamata na kumuongoza kwenye pikipiki aliyokuwa amepaki kisha kupiga hatua na kumpiga risasi kisha kutupa silaha na kukimbia Ndugu wa marehemu wametoa kauli hawapo tayari kupokea mwili na kuuzika licha ya polisi waliwasihi kufanya hivyo  Chanzo: Azam Tv
0 comments :
Post a Comment