Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, March 22, 2016

Mabasi ya mwengo kasi kufanyiwa majaribio wiki hii idadi ya mabasi itakuwa 30-50.soma zaidi.

Wataanza na mabasi kati ya 30 – 50 ambayo
yatapita kwenye njia zote za mradi huo. Zoezi
hilo litafanyika ili watumiaji wengine wakiwemo
waendesha daladala, bodaboda na watembea
kwa miguu waweze kutambua kuwa njia ya
mabasi yaendayo kasi si ya kwao, hivyo waanze
kuzoea,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Machi
22, 2016) wakati alipofanya ziara ya ghafla katika
Soko la Kimataifa la Samaki la Feri iliyokuwa na
lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi
sokoni hapo na kukagua ujenzi wa ukuta
unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo
kasi.
Waziri Mkuu ambaye ametembelea soko hilo
kuanzia saa 5:10 hadi saa 5:54, alitoa jibu hilo
wakati akijibu maombi ya mfanyabiashara mmoja,
Bw. Sharifu Ramadhani ambaye alisema
wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya usafiri kwa
vile mabasi mengi yanaishia Mnazi Mmoja.
“Mabasi yanaishia Mnazi Mmoja na huku ni mbali
kwa hiyo tunalazimika kutembea kwa miguu kwa
sababu kukodi taxi ni gharama kubwa,” alisema.
Akifafanua kuhusu hatua iliyofikiwa kwenye
utekelezaji wa mradi huo, Waziri Mkuu alisema:
“Hivi sasa wanakamilisha ufungaji wa mitambo
ya kukatia tiketi ambapo abiria atakuwa na kadi
kama za benki ambayo anaijaza fedha halafu
anapita kwenye mashine, kiasi cha nauli
kinakatwa halafu anaingia kwenye basi,
hakutakuwa na muda wa kukata tiketi.”
Alisema tatizo la usafiri kwa wafanyabiasha wa
feri litakwisha hivi karibuni baada ya mabasi
hayo kuanza.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top