Anna kilango Atenguliwa ukuu wake wa mkoa shinyanga..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli
ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Anna kilango Malecela kuanzia
leo.
Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango
Malecela kutungaza kwenye vyombo vya
habari kuwa mkoa wake hauna watumishi
hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu
kufanya uchunguzi wake na kubaini
kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika
awamu ya kwanza na awamu ya pili ya
uchunguzi bado inaendelea.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati
akipokea hundi ya shilingi bilioni sita
zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya
kubana matumizi kwa ajili ya kununulia
madawati Rais Magufuli ameeleza
kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza
Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa
Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.
Chanzo: ITV
0 comments :
Post a Comment