Breaking News
Loading...

Advert

Monday, April 11, 2016

Mgodi wa Acacia baada ya kukwepa kulipa kodi sasa kulipa kodi ya sh. billion 40 mwaka huu.

Baada ya kutuhumiwa kukwepa kodi kwa
miaka mitatu mfululizo, kampuni kubwa ya
uchimbaji madini ya Acacia imesema
inatarajia kulipa kodi ya zaidi ya Sh40
bilioni mwaka huu wa fedha.
Mwishoni mwa Machi, Baraza la Rufaa za
Kodi (TRAT) iliitaka African Gold Mine
(kwa sasa Acacia) kuilipa Serikali kodi ya
Dola za Marekani 41.25 milioni (zaidi ya
Sh89 bilioni), lakini kampuni hiyo ilikata
rufaa na shauri hilo linasubiri uamuzi wa
Mahakama ya Rufaa Tanzania.
Acacia inayomiliki Kampuni tatu ndogo za
Bulyanhulu Gold Mining, North Mara na
Pangea Minerals zinazoendesha shughuli
zote za mapato ya mchimbaji huyo
mkubwa kuliko wote nchini ambaye
anaelezwa kukwepa kodi ya zuio la
malipo ya gawio kwa wanahisa wake.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo,
Bradley Gordon ambaye aliwasili jana ili
kutembelea miradi hiyo na kuzungumza
na wafanyakazi wake, alisema Acacia
bado haijaanza kutengeneza faida za
kulipa kodi ya Mapato ya Kampuni kwa
kuwa bado haijarudisha mtaji wake wa
awali.
“Pamoja na kwamba tunatengeneza faida
kwa jumla, hiyo haitozwi kodi kwa sababu
bado hatujarudisha mtaji wa Dola za
Marekani 3.8 bilioni. Mkataba wetu na
Serikali ya Tanzania unaonyesha kuwa
tutatakiwa kuanza kufanya hivyo kuanzia
mwaka 2018,” inasomeka sehemu ya
taarifa iliyotolewa na Gordon.
Makamu wa Rais wa Acacia, Deo
Mwanyika alisema kuwa kampuni hiyo
inaanza kulipa kodi ya mapato mwaka
huu baada ya kurejesha mtaji wake
iliyowekeza kupitia kampuni yake ya North
Mara. “Tumerudisha mtaji wetu na
makadirio yanaonyesha tunaweza kulipa
kodi ya Dola 20 milioni za Marekani (zaidi
ya Sh40 bilioni). Nusu ya kiasi hicho
tayari kimeshapelekwa TRA,” alisema.
Chanzo: Mwananchi

0 comments :

Post a Comment

Back To Top