Sasa unaweza kulima kilimo cha ufuta uondoe umasikini soko lipo sehem yoyote duniani.soma zaid.
Tanzania imetajwa kuongoza barani Afrika katika
uzalishaji wa zao la ufuta,huku ikiwa ya tatu
duniani katika uzalishaji wa zao hilo ikitanguliwa
na nchi ya Mayami na India juhudi ambazo
zimetokana na taasisi ya utafiti wa mbegu
(Naliendele) kugundua aina nane za mbegu bora
za ufuta nakuonyesha kufanya vizuri nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mbegu na
azao ya kilimo kanda ya Kusini -naliendele Dokta
Omar Mponda amesema takwimu za Shirika la
Chakula Duniani zinaonyesha kuwa Tanzania kwa
sasa inazalisha zao la ufuta tani laki tatu na
sitini elfu,kwa Afrika ikifuatiwa na Nigeria.
Amesema mafanikio hayo ni makubwa
ukilinganisha na kipindi cha nyumba ambacho
kiwango cha uzalishaji kilikuwa tani 30,hivyo
kuna kila sababu ya kujivunia ugunduzi wa
mbegu mpya ambazo zimekubalika kwa
wakulima na kufanya vizuri katika mikoa yote.
nchini.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa zao la
ufuta katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi
wameonyesha kufanya vizuri katika kilimo cha
ufuta kwa kutumia mbegu mpya ikiwemo lindi
2002 iliyoonyesha mafanikio kwa wakulima
wadogo, wakati na wakubwa wa zao hilo la ufuta.chanzo itv.
0 comments :
Post a Comment