Breaking News
Loading...

Advert

Monday, April 11, 2016

TRA wawaburuza mahakani leo wachina kwa udanganyifu wa matumizi ya EFDs.


Wafanyabiashara watatu wa kichina
wamehukumiwa kulipa faini ya shilingi 4,000,000
kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya
udanganyifu katika matumizi ya Mashine za Kodi
za kielektronik (EFDs) kinyume na kanuni za
matumizi ya Mashine za Kilektronik za Kodi.
Wafanyabiashara hao walifikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala tarehe 11
Aprili 2016 kwa ajili ya kesi yao kutajwa.
Akisoma mashitaka, Mwendesha Mashtaka na
Wakili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Marcel Busegano, alisema washtakiwa Liu
Songyue, Liu Pengfei na Jiang Zedong walitenda
kosa hilo tarehe 12 Machi maeneo ya Tabata
Shule Dar es Salaam wakiwa na nia ya kukwepa
kodi kwa kutoa risiti ya EFD ya shilingi 200,000
kwa mteja aliyenunua bidhaa zenye thamani ya
shilingi 550,000.
Hakimu Hassan Mkasiwa aliwatia hatiani
wafanyabiashara hao kwa kufanya udanganyifu
katika mfumo au kwa Kamishna kinyume cha
Kanuni za matumizi ya EFDs.
Wanyabiashara hao kwa pamoja walikiri kosa na
Hakimu Mkasiwa akaamuru walipe faini shilingi
4,000,000 kila mmoja au kwenda jela miaka
mitatu kwa vile ni kosa lao la kwanza.
Wafanyabiashara hao walipa faini ya jumla
shilingi milioni 12.
Kufikishwa mahakani na kuhukumiwa kwa
wafanyabiashara wa Kichina ni muendelezo wa
kesi za wafanyabiashara mbalimbali zilizo
mahakamani kwa tuhuma mbalimbali za
ukwepaji wa kodi katika Mkoa wa Kodi wa Ilala.
Imetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao Makuu

0 comments :

Post a Comment

Back To Top