Obama ajuta kuipiga kivita libya na iraq.soma zaid.
Obama ni mnafiki sana kuliko marais
waliopita , Bush aliivamia Iraq na
kumng'oa Saddam Hussein kwa kisingizio
cha umiliki wa silaha za maangamizi ili
hali hazikuwepo Bush akutoa unafiki
wake kwakuwa alikuwa anajua anafanya
vile kwa maslahi ya taifa lake. 2011
Obama kafanya vilevile lakini kwa unafiki
wake anajutia leo wakati Syria anataka
kufanya kama Libya na ametumia miaka 5
sasa ila kwa msaada wa urus anaelekea
kushindwa.
Kwakuwa amekubali kinafiki kuwa
walifanya kosa kuivamia Libya na
kuangusha utawala wa Gaddafi basi
waache haraki zao za kumuondoa Assad
ili wasifanye kosa lingine maana
waswahili wanasema kutenda kosa sio
kosa bali kurudia kosa ndio kosa,
akifanya hivyo nitaona kuwa yeye sio
mnafiki.
Nimeona kuna wadau wanasema Obama
apelekwe ICC kufunguliwa mashtaka, ni
kweli lakini USA sio mwanachama wa ICC
alafu yeye ndio kiranja wa dunia hivyo
yupo juu ya maamuzi yote ya kimataifa
UN ilikataa uvamizi wa Iraq lakini Bush
akaagiza majeshi yavamie. Blair
mwenyewe alihojiwa na mamlaka za UK
kwa kutoa uamuzi wakupeleka vikosi Iraq
na ikaonekana kuna ukiukwaji wa sheria
za kimataifa lakini hakuna wa kumpeleka
ICC, Hilary Clinton naye aliwekwa kitimoto
juu ya uvamizi wa Benghazi lakini sasa
anagombea nafasi ya kuwakilisha chama
chake urais 2017. ICC haina meno kwa
maovu yanayofanywa na nchi za
magharibi, uvamizi wa Iraq na Libya ni
uhalifu wa kijeshi lakini ICC haiwezi
kemea kwa kuwa kuna double standards.
Marekani katika historia yake haijawahi
kuikalia nchi nyingine pasipo kuiacha
ikiwa haitawaliki, haigawanyiki na kuibuka
vikundi vikundi vinavyohasimiana . Hebu
angalia tangu waivamie Afghanistan na
Iraq hizi nchi hazitawaliki hadi sasa
utasikia Taliban, al Quida mara IS sijui Al
Nusra Front. Kila siku ni mabomu tuu na
serikali walizoziweka zinakosa ushawishi
na uungwaji mkono na raia hivo kuleta
vikundi vya kigaidi vinavyojaribu
kutengeneza dola kwakuteka na kukalia
ardhi.
Free Syrian army (FSA) kabla ya kujaribu
kung'oa utawala wa Assad kwa msaada
wa marekani wajitafakari sana huku
wakiangalia kilichotokea Libya kama case
study ya kitu wanachojaribu kufanya dhidi
ya serikali halali ya Syria, badala ya kujuta
baadaye kama wenzao walibya.
Naikubali sana ile kauli ya Donald Trump
aliposema dunia na mashariki ya kati
ingekuwa salama kama Gaddafi na
Saddam Hussein wangekuwepo. Alisema
ukweli mtupu bila kuficha kitu wala kuleta
unafiki wa kimarekani katika amani ya
mashariki ya kati na dunia kwa ujumla,
maana kila mtu anaona kinachoendelea
huko mashariki ya kati. Libya na Iraq
0 comments :
Post a Comment